Na Farida said, Morogoro.

Katika kusheherekea siku wa wanawake Duniani  Shirika la umeme Nchini TANESCO Mkoa wa Morogoro limeandaa mikakati ya kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme na kuwatoa hofu wanawake wa Mkoa huo ambao wamekuwa waathirika wakubwa wa Nishati hiyo.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Mandisi Fedgrace Shuma alisema anatambua changamoto zinazowakabili wanawake kipindi umeme unavyokatika ambapo amewahakikishia kumaliza tatizo hilo ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi zinazowaingizia kipata kwa uhakika.

Akiwa katika kituo cha makazi ya Wazee wasiojiweza cha Fungafunga Manispaa ya Morogoro wakati wa kutoa  zawadi kwa Wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wananwake Duniani Mhandisi Shuma amesema Tanesco Morogoro inatambua nafasi ya wazee kwenye jamii na kutumia siku hiyo ya wanawake Duniani kwenda kuwaona na kuwatia faraja Wazee hao.

Kwa upande wake Afisa Rasilimali watu TANESCO Morogoro Bi. Mery Marwa amesema pamoja na Serikali kufanya kazi kubwa ya kuwatunza Wazee hapa Nchini, pia wao kama watumishi wa TANESCO wamemeguswa kwenda kuunga mkono  juhudi za Serikali kwa kutoa zawadi mbalimbali zitakazowasaidia Wazee hao katika maisha yao ya kila siku.

Zawadi zilizotolewa kwa wazee hao ni pamoja na Magodolo, Sukari, Viatu, Mashuka  na Vitenge ambapo vyote kwa pamoja vimeghalimu takribani shilingi Milioni 2 huku Wazee  wakiwashukuru watumishi hao wa TANESCO Morogoro kwa kutambua thamani ya Wazee katika siku hiyo adhimu ya wanamke Duniani ambapo kimkoa ilifanika katika viwanja vya Jamuhuri katika Manispaa ya Morogoro.




 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...