Dar es Salaam. Machi 25, 2022. Mtandao namba moja Nchini kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo Tanzania wamezindua Duka jipya la kisasa litakalopatikana Palm Village Mall iliyopo kando ya barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni, Dar es Salaam  ambapo wateja wa Tigo sasa watapata huduma zote za Tigo katika Duka hilo.

Duka la kwanza la aina yake lililoboreshwa kwa njia ya kidijitali litatoa huduma zote zitakazojumuisha ubadilishaji wa SIM, uthibitishaji wa nambari, huduma za Tigo Pesa, huduma za Tigo Business, huduma za usajili wa SIM Card kwa kibayometriki, na skrini za kuonyesha vifaa kwa aina mbalimbali za simu na vifaa zinauzwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Uthmaan Madati amesema uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Tigo wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na kutimiza ahadi yake ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa na huduma kwa urahisi zaidi.

"Ahadi yetu kwa wateja ni kuwapa huduma za kibinafsi na kutoa suluhisho la duka moja kwa mahitaji yao yote. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma zetu kunatokana na hitaji la wateja kufuata mtindo wa maisha wa kidijitali. 

Mpango wetu ni kutoa suluhu zilizojumuishwa kama sehemu ya mkakati wetu wa kuendesha ujumuishaji wa kidijitali”

“Duka hili jipya lina eneo maalum la matumizi ambapo wateja wanaweza kupata fursa ya kufanya majaribio na kupata uzoefu wa bidhaa mbalimbali za Tigo kama vile simu za mkononi. 

Duka linapatikana kwa urahisi kwa wateja wanaotembelea duka la Palm village”,  aliongeza Madati.

Naye kwa upande waje Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. FATMA NYANGASA aliipongeza Tigo kwa dhamira yao ya kuwekeza rasilimali zake ili kuhakikisha wateja wanapata huduma za kiwango cha Kimataifa. 

"Huduma za wateja mara nyingi ndio kiini cha biashara ambacho hulenga kutoa huduma ya kipekee inayomwacha mteja anahisi kuthaminiwa na kuheshimiwa na Tigo ndiyo bora zaidi katika kuwekeza rasilimali zake katika kutengeneza uzoefu wa kukusudia mazuri kwa wateja," Alisema Mwegelo.

Tigo ni mwanzilishi wa uvumbuzi nchini Tanzania. Duka hili ni la 54 nchini na ni uthibitisho mwingine kwamba Tigo ni kinara katika utoaji wa huduma za  kidijitali kwa wateja wake.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...