Katika halakati za kuendelea kuwapa burudani watanzania bondia wa ngumi za kulipwa hapa nchini Twaha Kasimu maalufu kama Twaha Kiduku ameshinda pambano lake dhidi ya mpizani wake Alex Kabangu kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akiwa uwanja wa nyumbani Mjini Morogoro Twaha Kiduku alipata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki wake hali iliyomfanya bondia huyo kuibuka mshindi kwa kupata pointi zote za majaji watatu ambazo ni (80, 72), (79, 73) na (80, 72) na kumfanya kuibuka kidedea katika pambano hilo.

Pambano hilo la kuwania mkanda wa ubingwa ABU uzani wa Super Middle lenye raundi nane lililofanyika mkoani Morogoro katika Ukumbi wa Tanzanite na kushughudiwa viongozi mbalimbali wa serikali Pamoja na mamia ya mashabiki wa mchezo huo.

Pambano lilianza kwa mabondia wote wawili kucheza kwa tahadhari huku kila moja akimsoma mwenzake, ambapo pambano la pili, tatu, nne na tano Twaha Kiduku alianza kubadilisha mchezo kwa kuonyesha uwezo wake wa kurusha makonde kwa mpinzani wake na kuanza kuufanya ukumbi ulindime kwa shangwe.
Hadi raundi ya sita, saba na nane Twaha Kiduku alicheza kwa kujiamini kutokana na makonde makali aliyokuwa anarushia kwa mpinzani wake huku yeye akikwepa ngumi ambazo Kabangu alikuwa anarusha.

Akizungumza mara baada ya kumaliza pambano hilo, Twaha Kiduku alisema siri ya ushindi huo ni nidhanmu,jitihada za mazoezi na kumuweka mbele mungu kwenye kilapambano lake analocheza ndani na njee ya nchini.

"Nashukuru wakazi wa Morogoro na vitongoji vyake kwa kuja kunipa sapoti, pia uwingi wao leo ukumbi ndiyo imesababisha kupata ushindi huu, " alisema Kiduku.
Aliongeza kusema kuwa mpinzani wake alikuwa hana madhara yoyote japokuwa kuna muda alikuwa narusha makonde ambayo alikuwa anayakwepa.
"Sikutaka kuwaangusha watanzania na wana Morogoro ndiyo maana nilicheza vizuri na kwa akili kubwa, kusikiliza yale kocha angu alikuwa ananifundisha, " alisema Kiduku.

Kwa upande wake bondia, Alex Kabangu alisema ushindi huo alipaswa kupewa yeye ila kwakua Twaha Kiduku yupo kwao ndiyo sababu ha kupewa ubingwa huo.
"Japokuwa tanzania kuna joto ila haikuwa tatizo kwangu kucheza kwa weledi, lile pambano niliona ushindi ni wa kwangu kabisa, lakini sio zote mchezo kwao hutunzwa, " alisema Kabangu.

Kabla ya pambano hilo kulitangaliwa na mapambano mengine ya utangulizi yalioleta amshaamsha ukumbini huku mashabiski wakisuri makali wa ngumi kupanda ulingoni.

Katika pambano hilo hali ya ulinzi katika ukumbi huo uliimarika sana uliopo hapo kwa kuwa na idadi kubwa ya polisi ambao walianza kulinda kuanzia lango kuu la kuingia katika Ukumbi wa Tanzanite.

Kutokana na ulinzi huo hali ya utulivu katika ukumbi huo ulikuwa shwari huku wakazi wa Morogoro na vitongoji vyao walifurahia burudani ya masumbwi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...