Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UBALOZI wa Ufaransa nchini pamoja na Umoja wa Ulaya umesema zinasimama na Ukraine katika kuhakikisha ya kwamba vita baina ya Ukraine na Urusi inamalizika kwa njia ya mazungumzo ili kuepuaka madhara zaidi yanayoweza kutokea

Hayo yamesemwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzaia Najil Hajloui pamoja na mabalozi wengine walioko nchini ambao nchi zao ziko kwenye Umoja wa Ulaya( EU.)

Akitoa taarifa ya Ufaransa na Umoja wa Ulaya ,Balozi Nabil Hajloui amesema Machi 2,2022 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio ambalo linaitaka Urusi kusitisha mara moja matumizi ya nguvu dhidi ya Ukraine katika kura iliyoidhinishwa kwa wingi na nchi 141 ikiwa ni pamoja na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya huku nchi tano zikipinga na nchi 35 kuacha kupiga kura Kati ya wanachama 193 wa Jumuiya.

Amesema Ufaransa na Umoja wa Ulaya zilijiunga karibu na Jumuiya zima ya Kimataifa katika kulaani vikali mashambulizi ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine anbapo ni shambulio kubwa zaidi juu ya Usalama wa Ulaya katika miongo kadhaa.

"Kukabiliwa na vita vilivyoanzishwa na Urusi bila uchokozi wowote na ukiukwaji mkubwa wa sheria za Kimataifa na ahadi zake zote,nchi 27 wanachama wa EU zimepitisha vikwazo vikubwa dhidi ya Urusi . Jumuiya inasikitisha na matumizi makubwa ya nguvu yanayotumika kuishambulia Ukraine,"amesema wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari akiwa na viongozi kadhaa wa Umoja wa Ulaya.

Ameongeza kuwa EU imeamua kuweka vikwazo vya moja kwa moja kwa watu wanaohusika na maamuzi yanayohusiana na vita lakini pia mfumo wa kiuchumi wa umma na wa kibinafsi wa Urusi ambao unaunga mkono juhudi hizo za vita na kwamba katika upande wa kifedha Urusi iko karibu kuondolewa kwenye masoko ya kifedha.

"Vikwazo hivyo pia vitakuwepo katika kuzuia Uwekezaji wote katika sekta ya nishati ya Urusi na utangazaji wa vyombo vya habari ambavyo vinarudisha propaganda za vita vya Urusi katika EU. Tayari vikwazo hivyo vimeanza kufanya kazi,"ameongeza Balozi Nabil .

Aidha amesema EU iko tayari kuongeza shinikizo zaidi ili kuongeza ukali wa vita kwa Urusi ili kuifanya nchini hiyo kuamua kusitisha mapigano na kufikia mazungumzo kama Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alivyotangaza katika mkutano wa wakuu wa nchi za Ulaya wa Versailles Machi 10-11 mwaka huu.

Katika taarifa ya Ufaransa na Umoja wa Ulaya inaeleza wanachama wa EU wanaunga mkono ufunguzi wa uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai katika mashambulizi y Urusi na kisababisha majeruhi ya raia.Mahakama ya Kimataifa ya Haki iliamuaru Urusi kusitisha uvamizi nchini Ukraine." Hata hivyo Rais Emmanuel Macron anaendelea na mazungumzo na Vladimir Putin ili kupata suluhisho la amani katika mgogoro huo.

Wakati huo huo Balozi na Nabil pamoja na Umoja wa Ulaya wanatoa ombi kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kutoa kauli kwa Urusi ili iwezeshe kusitisha vita dhidi ya Ukraine na kwamba nchi za Afrika zinatambua madhara yanayopatikana kutokana na vita hiyo.

Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya wameeleza kuna maelfu ya raia kutoka Mataifa mbalimbali wamelazimika kukimbia makazi yao na wengine kuacha shughuli zao na miongoni mwao wamo walioacha masomo kwasababu ya vita inayoendelea Ukraine.

Balozi wa Umoja wa Ulaya Manifredo Fanti (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano huo akieleza jitihada zinazofanywa na Umoja huo kuhakikisha vita ya Ukraine na Urusi inamalizika.
Balozi wa Poland nchini Tanzania Krzysztof Buzaliski (katikati) akizungumza katika mkutano huo kuelezea namna ambavyo nchi yake ilivyojitolea kuhakikisha wakimbizi wanaokimbia vita na kuingia poland wanapokelewa na kupewa hifadhi.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Najil Hajloui (katikati) akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusu mapigano yanayoendelea baina ya Ukraine na Urusi . (kushoto), ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manifredo Fanti, na (kulia), ni Balozi wa Poland nchini Tanzania Krzysztof BUZALISKI. Mkutano huo umefanyika  katika Makazi ya Balozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania.
Baadhi ya Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano huo umefanyika katika makazi ya Balozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia taarifa inayotolewa na Mabalozi wa Umoja wa Ulaya kuhusuMsimamo wa nchi zao kuhusu mapigano yanayoeendelea kati ya Ukraine na Urusi.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...