Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) leo Machi 8,2022 imesaini mkataba na Kampuni ya Arqes Africa Architechs & Interior Designesers kwaajili ya kusanifu majengo ya Kituo cha Kikanda cha Umahiri wa Tehama (RAFIC) kazi ambayo inatakiwa kuanza mara moja na kukamilika ndani ya miezi minne.

Kazi ambazo anatakiwa kufanya mshauri elekezi huyo ni pamoja na kutengeneza 'Master Plan' ya DIT Kampasi Kuu ya Dar es Salaam, kusanifu majengo ya RAFIC na kumsimamia mkandarasi wakati wa ujenzi. Thamani ya kazi hiyo ni Sh 756,539,200

Hata hivyo Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Prof Preksedis Ndomba ameomba kazi hiyo ikiwezekana ikamilike ndani ya miezi miwili ili kupatikana kwa mkandarasi na kazi ya ujenzi ianze mara moja.

Katika tukio hilo la kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Arch. Lazaro Peter ameahidi kufanya kazi hiyo kwa umahiri mkubwa na ikiwezekana anajitahidi kukamilisha kazi ndani ya miezi miwili.





















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...