Wakwanza kushoto ni mkurugenzinwa Drive Change Foundation Peter Valentine,akifuatiwa na Peter Mark kutoka nchini Ujerumani pamoja na baadhi ya wanakikundi waliopatiwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki
Muwezeshaji wa mafunzo kutoka nchini Ujerumani Peter Mark akiwa na baadhi ya wajumbe wa vikundi vilivyowezeshwa mizinga na Shirika la Drive Change Foundation,kwaajili ya ufugaji wa nyuki wilayani Arumeru.
Na.Vero Ignatus,Arusha
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Drive change Foundation mkoani Arusha imetoa mizinga 300 Vikundi vitano katika wilaya ya Meru ,yenye jumla ya shilingi mil 74, kwaajili ya mradi wa ufugaji wa nyuki,ambapo kila mzinga unatazamiwa kuvuna kg 15 za asali hivyo kwa mizinga yote itatoa jula ya kg 4,500 kwa miezi 6
Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika hilo Peter Valentine, amesema wanajihusisha na kuwawezesha vijana kiuchumi na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, ambapo mizinga hiyo wataiweka kwa pamoja moja eneo la Oldadai wilayani meru, kwaajili ya Shamba darasa,amesema kwa sasa wapo nusu ya mradi,hivyo unaotazamiwa kukamilika ifikapo julai 2022
Peter amesema kuwa vikundi hivyo vitano ,kila kimoja kimepewa mizinga 60,ambayo ni ya kisasa ,mara baada ya kuvuna asali hiyo watawasaidia kutafuta masoko, na wao wataipeleka sokoni kwa kupitia nembo zao wenyewe ,huku Shirika hilo likiendelea kufuatilia maendeleo katika vikundi vyao
Aidha ametoa wito kwa vijana na wanawake kutumia fursa iliyopo katika shirika hilo, kwaajili ya kujiunga katika mafunzo ya ufugaji wa nyuki,ambapo amesema wao wapo tayari kuwafundisha ili waweze kujikwamua kiuchumi
‘’Vijana wanaomaliza vyuo ni wengi sana ,wamebakia kuzunguka mitaani na katika ofisi mbalimbali wakitafuta kazi,na kazi zenyewe hakuna ,tunawashauri ipo njia mbadala itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi ambayo ni ufugaji wa nyuki,tunawaalika vijana waje sisi tupo tayari kuwasaidia na kuwapatia elimu hii kwaajili ya kujikwamua kiuchumi’’alisema
Alivitaja vikundi hivyo ni pamoja na Olea Group,Golden heart group,Old is gold,Christian girls na Meru youth group ,amesema vikundi vyote hivyo vimesajiliwa kupitia ngazi ya wilaya na vyote vipo chini ya Shirika la Drive Change Foundation
Alex Daudi ni Afisa miradi katika Shirika la Drive change Foundation alisema mafunzo hayo ni ya tatu kwa vikundi hivyo, wamewezakufikia vijana zaidi ya 100,na wamekuwa wakifanya mara kwa mara, ili kuwezesha mradi uwe endelevu,pamoja na kuwa na ufuatiliaji wa karibu
Amesema kuwa uwiano huo ukitumika vizuri wanaifikia jamii kwa upana zaidi ,na kuwasaidia vijana kutokujiingiza katika makundi yasiyofaa ,ikiwemo kuvunja sheria ya nchi ambayo yataharibu hatima yao ya baadae
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi cha Golden Heart Youth group Innocent Mlati kutoka Patandi lenye wajumbe 30, amesema kuwa mafunzo hayo ya ufugaji nyuki walianza kuyapata kuanzia mwaka 2021 kwa wiki moja,ambapo walipatiwa mizinga 60,kwasasa wameamua kuipeleka eneo moja ambapo wataimbambua mizinga hiyo kwa namba watakazoziweka
Amesema kuwa mafunzo hayo ya awamu ya tatu kwao yana mchango chanya kwao,kwani awali waliyapitia kwa haraka ila kwa sasa wamefundishwa kwa kina njia mbalimbali za ufugaji wa nyuki ,kutunza nyuki,kufuga ng’ombe,kilimo cha mbogamboga ambapo baada ya mafunzo hayo wameamua kutanua wigo zaidi kwaajili ya kuyatendea kazi.
Naye Aleni Sumari Katibu wa kikundi cha Olea group chenye wajumbe 15 wanajishughulisha na kilimo na ufugaji kilichopo kutoka Kijiji cha Nduruma kata ya Keri,amesema mafunzo hayo ufugaji wa nyuki kwa kisasa zaidi kwaajili ya kupata faida
Amesema kuwa mategemeo yao ni kuwa wazalishaji bira wa asali na kuuza kwenye masoko makubwa kwaajili ya kuwapatia faida kwenye shirika na kwao pia ,amewataka vijana wenzao kuacha kubweteka wafanye kazi kwa bidiii ili kujikwamua kimaisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...