Picha ya pamoja iliyowakutanisha Waandishi wa habari,Watafiti wabobezi na Wabunifu
Pichani Kulia anayeongea ni mratibu wa mafunzo kutoka (COSTECH)Deusidedith Leonard akitoa ufafanuzi katika warsha hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt Philibert Luhunga akizungumza katika semina ya siku nne jijini Arusha.

 
Na Pamela Mollel,Arusha

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuipenda nchi yao kwa kuwa wazalendo kwa kuandika habari ambazo zitajenga na sio za kugombana na serikali iliyopo madarakani badala yake watumie kalamu zao kusifia Nchi.

Rai hiyo ilitolewa machi 16/2022 na kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)Dkt Philibert Luhunga wakati akizungumza katika semina iliyowakutanisha waandishi,Watafiti na wabunifu Mkoani Arusha

Alisema kuwa sio vyema waandishi kuandika vibaya kuhusu serikali badala yake watumie kalamu zao kuandika mazuri yanayofanywa katika nchi yao

"Pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo katika nchi ya Marekani huwezi kuskia wala kuona waandishi wa nchi hiyo wakikosoa serikali yao zaidi sana utaona wakitumia kalamu zao kusifia"Alisema Dkt Luhunga

Aliongeza kuwa ni vyema waandishi wakaisemea serikali ya Rais Samia Suluhu kwa mambo makubwa anayofanya katika Nchi hii

Pia aliwakumbusha waandishi hao juu ya umuhimu wa kujiheshimu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kujiweka nadhifu ili watu wengine waipende taaluma ya uandishi wa habari

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka (COSTECH)Deusidedith Leonard alisema kuwa lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika taarifa za Sayansi Teknolojia na Ubunifu kwa lugha rahisi ili ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka

Alisema kupitia semina hizo wanategemea kupata ongezeko la makala pamoja na vipindi vinavyohusu Sayansi katika Redio,Televisheni,Magazeti na mitandao ya kijamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...