Wafanyabiashara wa Vinywaji
pamoja na watumiaji wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuhakiki Vinywaji
kwa kutumia app maalumu ya Hakiki stempu ili kutambuwa bidhaa feki
sokoni ambayo zinaweza kuleta athari kwa mlaji.
Akizungumza mjini
Babati Mkoani Manyara Balozi wa Kodi Edward Kumwembe amesema
application ya Hakiki stempu inauwezo wa kutambua uhalali wa bidhaa za
Vinywaji ambazo zipo sokoni ambapo mtumiaji atapaswa kuwa na Application
hiyo katika simu janja na kufanya uhakiki kwa kutumia simu yake kama
iwapo bidhaa hiyo inafaa kwa matumizi ya binadamu.
Kumwembe
amesema "kuna app maalumu ambayo inapatikana katika hizi simu za
smartphone ambazo Zina application au maarufu watu wanaita App ambayo
inahakiki ubora wa Vinywaji vyako, ambayo inahakiki kwa njia mbili wewe
ukiwa ni mnunuaji kutoka sehemu nyingine unaweza inahakiki Vinywaji
vyako lakini vilevilie wewe unapomuuzia mtu mwingine mteja naye anaweza
kuhakiki kwasababu wakati mwingine unaweza kununua kitu ambacho hakina
ubora lakini siyo kosa lako"
Aidha Kumwembe amesema lengo la
kuhakiki ubora wa bidhaa za Vinywaji ni kwa sababu kuna aina nyingi za
Vinywaji hivyo siyo rahisi kufahamu ubora wa Vinywaji hivyo.
Amesema
kwa kutumia mfumo huo wa app utaweza kupata taarifa sahihi kuhusu
ilipotoka bidhaa,ilipotengenezwa,na lini itaisha muda wake wa matumizi
hivyo kumfanya mlaji wa bidhaa husika kuwa salama.
Kwa Upande
wake muuzaji wa Vinywaji mbalimbali kutoka Mjini Babati Bw.Naingwa
ameishukuru mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kutoa elimu juu ya matumizi
sahihi ya kutumia application hiyo inayoweza kuhakiki ubora na uhalali
wa Vinywaji na kwamba itawasaidia kuepuka kununua bidhaa feki.
"Application
hii inafaida nyingi kwa sisi wafanyabiashara hasa pale tunapo kwenda
kununua Vinywaji kwani itatusaidia kutambuwa Vinywaji feki pamoja na
kufahamu ubora wa Vinywaji hivyo ili kumlinda mteja"alisema
Hata
hivyo maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu
wapo Mkoani Manyara kwa siku kumi katika kampeni ya walioiita Mlango kwa
mlango (Door to door) inayolenga kutoa elimu kwa Wananchi na
wafanyabiashara juu ya matumizi sahihi ya EFD machine,matumizi ya Hakiki
stempu inayolenga kutambuwa Vinywaji feki sokoni na msisitizo wa kutoa
na kudai risiti baada ya kuuza au kununua bidhaa.
Balozi wa kodi Bw. Edward kumwembe akifanya zoezi la Hakiki stamp
Balozi wa Kodi Edward kumwembe
Afisa wa TRA akitoa Elimu ya kodi
Home
HABARI
WAFANYABIASHARA WA VINYWAJI NA WATUMIAJI WATAKIWA KUHAKIKI VINYWAJI KUTUMIA MFUMO MAALUM 'APP' YA HAKIKI STEMPU KUTAMBUA BIDHAA FEKI SOKONI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...