WANAWAKE nchini wameshauriwa kutumia teknolojia mbalimbali za kisayansi katika shughuli zao za kila siku ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakiongezeka kila siku.
Mara nyingi mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakiwaathiri wanawake zaidi kuliko wanaume kwa sababu mambo yao mengi wanayoyafanya yameshikamana na mazingira, huvyo kama wakitumia ushauri, teknolojia mbali mbali basi wanaweza kuondokana na changamoto hizo mabadiriko ya tabia nchi na kuweza kupambana nazo.
Ushauri huo umetolewa leo Machi 9, 2022 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk Philbert Luhunga leo wakati wa hitimisho la siku ya wanawake duniani lililofanywa na wanawake kutoka Costech jijini Dar es Salaam.
" Leo tupo hapa tunahitimisha Siku ya wanawake duniani, lakini tutakuwa na mdahalo unaohusisha wanawake kujua jinsi gani wanaweza kupambana na changamoto hii ya mabadiliko ya tabia nchi," amesema
Amesema, shughuli nyingi za wanawake zinahusisha mazingira ambapo ametolea mfano kilimo na maji na kusema kuwa kwenye kilimo wajaribu kubadirisha mtindo wa zamani wa kulima waweze kutumia pembejeo za kilimo na vile vile watumie teknolojia ya nishati mbadala ili kuweza kuweza kupika na kuachana na ile ya BBC's n kizamani ya kukata kuni.
"Hapo zamani kuni na maji ni vitu vilivyokuwa vinapatikana kwa urahisi likini nishati ya kupikia mbadala inahitajika hivyo teknolojia mbali mbali zinahitajika.
Aidha amesema katika mdahalo huo wanawake wanajaribu kujadili namna gani watakabiliana na hizo changamoto za mabadiriko ya tabia nchi, na wamekuwa wazi kabisa kwa kumuangalia mwanamke kutoka kijijini mpaka anapokuwa hapa mjini.
Kwa upande wake Mbobezi wa masuala ya mazingira nchini kutoka E- Link, Shukuru Nyagawa amesema wanawake ndio wanaoathirika na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na athari zinazompata zinaweza kutokana na mvua, kwa kuwa na mvua nyingi hadi kuharibu mazingira au kuwa kidogo na kusababisha ukame unaochangia Uhaba wa maji.
" Athari zinazompata mwanamke kukiwa na mvua, ukame, kimbunga, mabadiliko ya mabadiliko ya tabia nchi yanaendelea kuongezeka kwa kazi. Taarifa zinaeleza joto limeongezeka tumefikia kwenye nyuzi joto 1.1 inawezekana ikafikia nyuzi joto 1.5 ifikapo 2030.
" Ikifikia huko kutakuwa na athari kuwa kwenye uchumi wa Jamii na wanawake ndio wanaoathirika zaidi," alisema.
Amesema kwenye ngazi ya kidunia kuna uhamasishaji wa kuangalia mwanamke anakuwa ni kiini cha mabadiliko na kusaidiwa.
Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Dk Magreth Samiji amesema wamebuni Mradi wa majiko ya sola ikiwa ni njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema wamefanya utafiti huo wa majiko baada ya kwenda wilaya ya Isimani Iringa na kukuta wanawake wanapikia masalia ya mahindi pamoja na vinyesi vya wanyama hivyo walitengeneza majiko 42 na kuyagawa.
Mapema Dkt Harun Makandi mratibu wa utafiti kutoka Costech amesema tume hiyo imekuwa ni mshauri mkuu wa serikali na wadau wengine katika mambo yanayohusu utafiti na ubunifu ambapo imekuwa ikisaidia kuandaa sera kuhusiana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na kuishawishi serikali ili kuitekeleza.
Mbobezi wa masuala ya mazingira nchini kutoka E-link, Shukuru Nyagawa akiwasilisha mada ya mabadiliko ya tabia nchi na athari wanazokutana nazo wanawake na namna ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo leo Machi 9, 2022 wakati wa hafla ya kuhitimisha siku ya wanawake leo jijini Dar es Salaam.
Wanawake kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) wakiwa katika picha ya pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...