Na Muhidin Amri,Nanyumbu

WANAWAKE wa kijiji cha Mkwajuni kata ya Mikangaula Halmashauri ya wilaya Nanyumbu mkoani Mtwara,wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya maji kujenga mradi mkubwa wa maji uliofanikisha kufikisha huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema,kabla ya mradi huo kujengwa walipata shida kubwa ya maji hali iliyosababisha kuhatarisha afya zao kwa kutumia maji kutoka kwenye vyanzo ambavyo sio salama.

Melina Lucas alisema,walilazimika kwenda mbali kufuata maji kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku, jambo lililorudisha nyuma maendeleo yao kwa kuwa walipoteza muda mwingi kwenda kutafuta huduma hiyo badala ya kufanya kazi za maendeleo.

Alisema hatua ya serikali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga mradi wa maji, imewapunguzia mzigo mkubwa na ugumu wa maisha na kuokoa ndoa nyingi kutokana na kufuata huduma ya maji mbali na makazi yao.

"kwa kweli tunamshukuru sana Rais wetu mpendwa Samia Hassan kwa kututua ndoo kichwani sisi wanawake wenzake,shida ya maji katika kijiji chetu ilikuwa kero kubwa hasa kwa wanawake ambao tulilazimika kuamka usiku kati ya saa 10 na 11 kwenda kutafuta maji kwa ajili ya familia zetu"alisema Melina.

Clara Simon,ameiomba Serikali kupeleka huduma nyingine za kijamii katika kijiji hicho ikiwamo nishati ya umeme ili wananchi waweze kutumia kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Katibu wa Jumuiya ya watumia maji Yasin Yahaya alisema,watahakikisha wanatunza mradi huo na miundombinu yake na kuwachukulia hatua watu wakaojaribu kuharibu mradi huo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kibindamu ikiwamo kilimo na kuchungia mifugo kwenye vyanzo vya maji.

Alisema, kwa sasa bei ya maji ndoo ya lita 20 ni shilingi 100 na ndoo ya lita 10 shilingi 50,hata hivyo alielezwa kuwa gharama hizo ni kubwa kwa sababu wanaendeshaji mradi huo kwa Jenerata linalotumia mafuta ya Dizel kusukuma maji kwenda kwenye makazi ya wananchi.

Ameiomba Serikali kupitia Shirika la umeme nchini (Tanesco),kuharakisha kupeleka nishati hiyo ili utumike kuendesha Jenereta na shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Simon Mchucha alisema,mradi wa maji Mkwajuni-Mikangaula- Changombe ulianza kutekelezwa mwezi mei 2020 na kukamilika Disemba 2021.

Alisema,mradi huo umegharimu Sh.milioni 391,935,498.45 na utahudumia wakazi 4,431 wa vijiji hivyo na umetekelezwa kwa kutumia wataalam wa ndani kwa mfumo wa force Akaunti.

Alisema,serikali kupitia Ruwasa itaendelea kujenga miradi ya maji katika maeneo yenye changamoto hiyo na kuwapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa kutoa ushirikiano mkubwa wakati wote wa ujenzi wa mradi.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mchucha,Ruwasa imedhamiria na imejipanga kutekeleza na kukamilisha miradi yote ya maji ili kumaliza kero ya muda mrefu kwa wananchi ambao wanalazimika kutumia muda mwingi kwenda kutafuta maji kwa matumizi yao ya kila siku.

Amewataka wananchi,kutunza mradi huo ili uwe endelevu na kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi kwa mwenzake ili uweze kuleta tija kwa vizazi vya sasa na baadaye.


mkazi wa kijiji cha Mkwajuni Halmashauri ya wilaya Nanyumbu mkoani Mtwara Magreth Edmund kushoto akitwishwa ndoo ya maji na Afisa Maendeleo ya Jamii Clever Paul kulia baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji safi na salama uliotekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Nanyumbu mkoa Mtwara.

Diwani wa kata ya Mikangaula Halmashauri ya Nanyumbu mkoani Mtwara Abdul Chiliwi kushoto akifungua koki katika kituo kimojawapo cha kuchotea maji kilichojengwa na wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Nanyumbo kwa lengo la kusogeza na kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa kijiji hicho,anayeshuhudia kulia Meneja wa Ruwasa wilayani humo Mhandisi Simon Mchucha.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mkwajuni wilayani Nanyumbu wakichota maji katika kituo kimojawapo kilichojengwa na Ruwasa kupitia mradi wa maji safi na salama wa Mkwajuni-Mikangaula-Chang'ombe uliotekelezwa na Ruwasa kwa gharama ya Sh.milioni 391,935,498.45 ambao utawanufaisha takribani wakazi 4,431 wa vijiji vitatu vya kata ya Mikangaula.

Kaimu Meneja wa wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijijini)Ruwasa)wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara Mhandisi Simon Mchucha katikati akiwa katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Ruwasa mkoa wa Mtwara na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya watumia maji ya kijiji cha Mkwajuni kata ya Mikangaula .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...