Na Mwandishi Wetu - Geita
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kasala amewataka Watanzania kusimamia ukweli na haki katika kumuenzi Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli.
Askofu Kasala ametoa rai hiyo leo Alhamisi Machi 17, 2022 kwenye ibada ya misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati John Magufuli inayofanyika katika uwanja wa Magufuli Chato.
Amesema Hayati Magufuli alisimamia ukweli na kile anachokiamini hivyo kuwataka wananchi na viongozi kushuhudia ukweli huo katika maisha yao.
“Tukisimamia ukweli na haki, marehemu wetu wanazo dhawabu walizoondoka nazo, tuko tayari kuyachukua hayo kuwa kama dira ya maisha yetu? amesema
Askofu Kasala amesema kila mmoja kwa nafasi yake awe na kiu ya haki katika maisha na kujitoa kuietea.
“Njaa ya haki ni pale katika ubinadamu wako unaposema siwezi kushuhudia kuona mtu akiwa anaonewa, ananyanyaswa na kudhulumiwa,
Maudhi kwa ajili ya haki yanakuja pale tu mmoja anaposimamia haki bila kijibakiza na kusimamia haki ni kujitoa sadaka lakini bora niudhiwe lakini haki itendeke” amesema Askofu Kasala
Amewataka wananchi kuzidi kumombea toba kwa Mungu Hayati Magufuli
"Tunapokua kwenye ibada hii tunapaswa kukumbuka huyu alikua kiongozi wetu na kuna mema mengi alitenda akiwa na sisi na kama imani ya kanisa inavyo tuambia tuendelee kumuombea toba ili Mungu ampokee mbinguni" amesema Askofu Kasala.
Ibada hiyo imehudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hasani na viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi, wastaafu na wananchi.
Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hassein Mwinyi na mkewe pamoja na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango.
Wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson, Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula, Waziri wa Tamisemi, Inocent Bashungwa, Mbunge wa Jimbo la Ismani, William Lukuvi pamoja na Balozi Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole.
Pia wapo viongozi wastaafu wakiwamo Makamu wa Rais wa awamu ya nne, Ghalib Bilali, mawaziri wakuu wastaafu Joseph Warioba na Mizengo Pinda.
Wengine ni aliyekuwa Spika wa Bunge, Anna Makinda mke wa Rais wa awamu ya tatu hayati, Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa.
Wakati wa ibada hiyo ikiendelea mvua kubwa imenyesha huku mamia ya wananchi waliopo kwenye uwanja huo wakiendelea kushiriki kwenye ibada.
Baada ya ibada Rais, viongozi pamoja na familia wataambatana kwenda kwenye kaburi la Hayati Magufuli kwa ajili ya kuweka mashada ya maua.
Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, mwili wake ulizikwa Ijumaa Machi 26, 2021 katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato Mkoa wa Geita katika makaburi ya familia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...