Na.Khadija Seif,Michuzi TV

WATAYARISHAJI wa Kazi za Filamu wameshauriwa kutengeneza Filamu zitakazoendelea kutangaza Tamaduni za Kitanzania Ili kuendelea kuonyesha vitu vya asili zaidi kuliko kutangaza Tamaduni za nje.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo amesema Serikali kupitia Bodi ya Filamu itaendelea kufanya Kazi kwa karibu na Wadau wa Filamu hasa katika kupanua wigo wa Masoko ya Filamu ili kukuza na kuendeleza Tasnia Kimataifa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa uzinduzi wa Huduma ya upatikanaji wa Filamu Kidijitali ya Vidotv Tanzania, inayomilikiwa na VIDO Media Marchi 10 mwaka huu katika Ofisi za Bodi Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kilonzo amesema Wadau wa Filamu wana fursa kubwa ya kuuza na kukuza kazi za Filamu kwa njia mbalimbali za kimtandao ili kuwafikia kwa urahisi Wateja wa ndani na nje ya Nchi.

“Hili ni dirisha lingine linalopanua wigo wa fursa za masoko ya Filamu na kazi za Wadau wetu, nitoe wito kwa Wadau kuandaa Filamu bora zitakazoweza kuuzika na kufikia masoko ya Kimataifa,” alisema Dkt. Kilonzo

Mkurugenzi Mtendaji wa Vido App Justine Kisai amesema Kampuni hiyo imefikia hatua hiyo ili kuendana na Kasi ya Mabadiliko ya Kiteknolojia ambayo yanaenda sambamba na Matumizi ya simu za mikononi katika maeneo mengi kwa watu wa makundi mbalimbali.

Hata Hivyo, upatikanaji huo wa Filamu kwa njia ya simu za mkononi utaongeza biashara kwa Watayarishaji na kwa Wateja wa Filamu kwa gharama ya Shillingi 500.

“Haya ni mabadiliko yatakayoleta faida kwa Wadau wa Filamu hasa kwa kuzingatia kuwa Filamu ni biashara, Filamu ni ajira na Utamaduni wetu. Hivyo, tutumie fursa hii ya kukuza Tasnia hii kwa kujiunga kwa Shillingi 500 tu,”

Kisai amesisitiza kuwa Filamu zitakazokuwa zinapatikana katika huduma hiyo ni zile zilizofuata taratibu za uandaaji wa Filamu na kufanyiwa uhakiki na Bodi ya Filamu.

"kwa kufanya hivyo kutasaidia katika kukuza maadili na Tamaduni za Kitanzania kwani tuna amini kuwa Filamu yoyote Ili ipewe nafasi ya kuwa sokoni ni lazima iwe imekaguliwa na bodi ya Filamu na kupewa dhamana na daraja "

Pia ametoa Rai Kwa Waandaji wa Filamu kuendelea kuzingatia uandaaji wenye mazingira na maisha halisi ya Kitanzania ili kukuza soko na tamaduni za Tanzania.

Kwa upande wake Msanii wa Filamu nchini Kulwa Kikumba maarufu kama "Dude" amepongezi uongozi mzima wa app hiyo yenye lengo la kukuza na kusambaza kazi za Filamu nchini.

Pia ameongezea kuwa Kwa sasa Filamu yake iliyotikisa miaka ya nyuma "Bongo dar es salaam" itapatikana rasmi kwenye app hiyo hivi karibuni.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo akifafanua zaidi kuwa Serikali kupitia Bodi ya Filamu imedhamiria kuwa karibu na wadau wa Filamu Ili kupanua wigo Mpana wa Masoko ya kazi za Filamu nchini

Msanii wa Filamu nchini Kulwa Kikumba maarufu kama "Dude" akizungumza machache na kuwakumbusha wadau na Mashabiki wa "Bongo dar es salaam" kukaa tayari kwani kupitia app hiyo ya "Vido" itaanza rasmi kuonyesha Filamu yake

sehemu ya wahudhuriaji wa hafla fupi ya uzinduzi wa app ya "Vido" ambayo itatumika kusambaza kazi za Filamu ndani na nje ya nchi Kwa kutumia Mfumo wa Filamu kiganjani Kwa kutumia Mitandao ya simu ambapo mteja ataweza kupakua app hiyo Mtandaoni na kulipia shilingi mia 5 na kumuwezesha kutazama Filamu ipendayo ambayo itazingatia maadili ya Kitanzania na utamaduni Kwa ujumla

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...