Katibu Msaidizi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Ndug. Salvatory Kaiza amewaasa watumishi wanawake kutoka katika taasisi za umma na binafsi za elimu ya juu kukemea na kufichua vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike, ameyasema hayo leo tarehe 03/03/2022 katika mafunzo ya nidhamu na utaratibu wa undeshaji wa mashauri ya nidhamu sehemu za kazi yaliyoandaliwa na Chama cha wafanyakazi taasisi za elimu ya juu THTU - wanawake taifa  katika ukumbi wa maktaba ya  Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Dar es salaam.

Ndg. Salvatory Kaiza amesema “nidhamu ni swala la muhimu sana kwa watumishi wa umma ili kufikia malengo ya Taasisi, ni vyema wafanyakazi kuzingatia,sheria taratibu na kanuni mahali pa kazi ili kufanikisha utendaji wa kazi katika taasisi,kulinda utumishi wetu na tumalize utumishi wetu salama pia kuwalinda watoto wetu hasa wakike walioko vyuoni” amesema Salvatory Kaiza.

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Eventus Mugyabuso amepongeza mafunzo hayo kwani Mwanamke ndiye mhanga mkuu pale mtumishi wa Umma yeyote anapo adhibiwa akifanya makosa iwe yeye mwenyewe au iwe familia, hivyo ni jambo jema sana kwa mafunzo haya kuandaliwa na wanawake wa THTU Taifa ambaye Mwenyekiti wake ni mhadhiri msaidizi kutoka hapa katika Taasisi yetu ya Ustawi wa Jamii. 

Kwa upande wake Prof Sotco Claudius Komba Makamu Mkuu wa Taasisi Taaluma, amewakaribisha wafanyakazi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na watumishi wanawake wa Taasisi za elimu ya juu waliofika kushiriki  katika mafunzo hayo ambayo yatasaidia katika ustawi wa nidhamu kazini na amewashukuru wote kwa kuja kupata mafunzo haya.

“Nawakaribisha sana katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii na tunashukuru kwa kuja kuendesha mafunzo haya kwenye Taasisi yetu, tunaamini mafunzo haya yatatupa mwangaza kuhusiana na nidhamu kwa wafanyakazi” amesema Prof Komba.

Kaimu mratibu Msaidizi kamati ya wanawake THTU Bi Roselyne Mathew Massam amesema mafunzo haya yameratibiwa na chama cha wanawake THTU kuelekea kwenye maazimisho ya siku ya wanawake Duniani yenye lengo la kusaidia watumishi kuelewa umuhimu wa nidhamu mahali pa kazi, kupunguza migogoro kazini na ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.

Aidha Bi Roselyne Massam ameomba Tume ya Utumishi wa Umma kuongeza wafanyakazi wanaoshughulikia mashauri ya nidhamu sehemu za kazi ili kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.

“Tunaomba tume iongeze watendaji ili kusaidia kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi,mashauri mengi yanachukua muda mrefu na inachukua muda mrefu kwa mfanyakazi kurudishwa kazini” amesema bi Roselyne.

Mafunzi hayo ni ya siku moja waliyo andaliwa na wanawake wa THTU kuelekea kilele cha siku wa Mwanamke Duniani tarehe 8 Machi 2022.

Bw. Salvatory Kaiza akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi za Umma na binafsi wakati wa mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyofanyika tarehe 03/03/2022 katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, kijitonyama Dar es salaam.
Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Eventus Mugyabuso akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu,waliohudhuria mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na watumishi wanawake wa chama cha watumishi wa Elimu ya Juu na kufanyika katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, kijitonyama Dar es salaam.
Bi. Roselyne Mathew Massaum akisoma risala iliyoandaliwa na kamati ya wanawake THTU,wakati wa mafunzo ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na  watumishi wanawake wa taasisi za Elimu ya Juu wa chama cha watumishi wa Taasisi za Elimu ya Juu.

Dkt Paul Loisulie mwenyekiti wa THTU Taifa akichangia mada wakati wa mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na watumishi wanawake wa chama cha watumishi wa Taasisi ya Elimu ya Juu. Yaliyofanyika katita ukumbi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...