WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na balozi wa Norway nchini Tanzania na kumueleza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania walipokutana Leo tar. 7 Machi, 2022.

Dkt. Kijaji ameishukuru serikali ya Norway kwa ushirikiano na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Dkt. Kijaji amemueleza balozi wa Norway kuwa nchi ya Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa lengo la kuvutia wawekezaji na kuhakikisha kuwa wawekezaji waliopo wanafaidika na kupanua biashara zao.

Ameongeza kwa kusema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua milango kwa wawekezaji kuja nchini Tanzania kuwekeza kwenye sekta mbalimbali hususani viwanda vya kuchakata bidhaa za kilimo, viwanda vya dawa na Vifaa tiba, Nishati na mbolea.

Dkt. Kijaji Amesema kuwa nchi yetu inafanya kazi na sekta binafsi Kwa karibu Sana ndio maana Mhe. Rais Samia amekuwa nao katika kila ziara ili kuwajengea uwezo sekta binafsi kwani ndio injini ya uchumi wa nchi. 

Naye balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania sambamba na maboresho makubwa yaliyofanyika na yanayoendelea  ili kuhakikisha Mazingira ya uwekezaji na biashara yanakuwa rafiki.

Balozi Elisabeth Amesema kuwa mazingira ya Uwekezaji nchini Tanzania yameboreka na hiyo ndio imewavutia zaidi nchi za ukanda wa Nordic kujipanga Kwa ajili ya kuwekeza nchini.

Wawekezaji kutoka katika nchi za Norway na Sweden wapatao 100 wapo tayari kuja nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo  mafuta na gesi, viwanda vya mbolea, Nishati na Viwanda vya kusindika mazao ya kilimo. 

Dkt. Kijaji alimshukuru sana Mhe. Balozi kwa ujio wake na kuahidi kuwa yuko tayari kufanya kazi na yeye kwa ukaribu na kuishukuru Serikali ya Norway kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwenye Nyanja mbalimbali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...