Dkt. Damas Ndumbaro ambaye niWaziri wa Maliasili na Utalii leo Machi 8, 2022 amekutana na wadau wakubwa wa Utalii kutoka nchini Uhispania na kufanya nao mkutano kuhusu fursa mbalimbali za utalii na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.
Mkutano huo umeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania - Paris unaowakilisha pia Uhispania pamoja na Shirika la Utalii Duniani.
Wadau hao, walionyesha ari kubwa ya kuendelea kushirikiana na Ubalozi ili kupeleka idadi zaidi ya watalii kutoka Uhispania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...