Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na katika kikao cha kupitia na kujadili maelezo ya randama kwa mwaka 2022/23 pamoja na taarifa za utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2021/22 kwa mafungu yaliyo chini ya Wizara hiyo. Kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Naibu Waziri, Jumanne Sagini, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Kayuni (kulia), akimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha kupitia na kujadili maelezo ya randama kwa mwaka 2022/23 pamoja na taarifa za utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2021/22 kwa mafungu yaliyo chini ya Wizara hiyo katika Kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mkuu, Bryton Monyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, akizungumza na katika kikao cha kupitia na kujadili maelezo ya randama kwa mwaka 2022/23 pamoja na taarifa za utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2021/22 kwa mafungu yaliyo chini ya Wizara hiyo. Kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni, na kushoto ni  Katibu Mkuu, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia meza kuu), akimsikiliza Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Boniface Kipomela, alipokuwa anawasilisha maelezo ya randama kwa mwaka 2022/23 pamoja na taarifa za utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2021/22 kwa mafungu yaliyo chini ya Wizara hiyo katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wanja Mtawazo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...