Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)
amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa
Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Baada ya kupokea nakala ya hati hizo Balozi
Mulamula amemuahidi Balozi mteule ushirikiano katika utekelezaji wa
majukumu yake ya kibalozi wakati wote atakaokuwepo nchini.
“Leo
nimepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa
Malawi na tumefarijika kwa Mhe. Rais Chakwera kumteua Balozi huyu mara
baada ya Balozi wa awali kumaliza muda wake wa uwakilishi, hii ni ishara
ya uhusiano wa karibu, undugu na urafiki uliopo baina ya Tanzania na
Malawi,” amesema Balozi Mulamula
Kwa upande wake Balozi Mteule wa
Malawi Mhe. Andrew Kumwenda amesema kuwa Malawi na Tanzania siku zote
zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na jukumu langu hapa kama
Balozi ni kuhakikisha uhusiano huu unazidi kuku ana kuimarika.
“Tanzania
inatekeleza Diplomasia ya Uchumi na vivyo hivyo Malawi………kwa hiyo sisi
wote tuna lengo moja, na nitahakikisha Tanzania na Malawi zinashirikiana
kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande mbili,” Amesema
Balozi Kumwenda.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula akipokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule
wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula akiongea na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda
leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi
Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda akimfafanulia jambo Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula mara baada ya kuwasilisha nakala ya Hati za Utambulisho
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew
Kumwenda yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe.
Andrew Kumwenda
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda katika
picha ya pamoja na maafisa walioambatana nao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...