Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara yake inakusudia kuimarisha maabara na kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa sekta ya afya ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza na Ugeni kutoka Shirika la Misaada Marekani ambao wanawakilisha OGAC na CDC huko ofisini kwake Mnazi Mmoja amesema kupitia Shirika hilo watakuwa mstari wa mbele katika kupambana na maambukizi ya UKIMWI.
Amesema wafanyakazi watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti ili kuongeza kiwango cha utoaji huduma na kuimarisha sekta ya afya nchini.
“Katika kuwajenga katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ni kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kufanya utafiti ambao utasaidia katika kutoa huduma bora kwa jamii”, alisema Waziri Mazrui.
Ameeleza kuwa kupitia Shirika hilo wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na UKIMWI nchini, hivyo ameomba kuwepo na ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza janga hilo.
"Ni kweli hivi sasa tuna waathirika wa UKIMWI 7600, waathirika 400 kwa mwaka 2020 hadi 2021 hichi si kiwango kidogo katika Nchi yetu", amesema Waziri Mazrui.
Waziri Mazrui amesisitiza jamii kuongeza juhudi ya kutoa ushauri kwa walioathirika wasiwaambukize wengine, kuwapatia matibabu kwa wale walioathirika ili waendelee kuishi vizuri.
Hata hivyo Waziri Mazrui amesema wapo katika ujenzi wa hospital 10 za Wilaya na moja ya Mkoa ambazo zina malengo ya kutoa huduma bora za afya kwa jamii na jukumu kuu la sekta ya Afya ni kuimarisha afya za wananchi.
Amefahamisha kuwa katika kupambana na maradhi ya kuambikiza Mke wa Rais Mama Maryam Mwinyi yupo mstari wa mbele katika kupambana na kupinga maambukizi ya UKIMWI nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ujumbe huo Michelle Chevalier amesema lengo la Shirika hilo ni kuweka mashirikiano ya karibu na sekta ya Afya katika mapambano ya kujikinga na maradhi ya UKIMWI, viashiria vya maradhi hayo pamoja na kuwapatia huduma waathirika.
Vile vile ameahidi kuweka mashirikiano katika suala zima la kuzuia maradhi ya UKIMWI na mengine makubwa yakiwemo Saratani kwa wanawake na watoto.
Home
AFYA
WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAKUSUDIA KUIMARISHA MAABARA NA KUWAPATIA MAFUNZO WAFANYAKAZI SEKTA YA AFYA KUTOA HUDUMA BORA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...