Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Arusha

WAMEMPOKEA kwa heshima!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya mamia ya wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho upande wa Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana.

Kinana amewasili mkoani Arusha akitokea mkoa wa Kilimanjaro ambapo ameendelea kufanya ziara ya kikazi yenye lengo la kuangalia uhai wa Chama pamoja na kupata fursa ya kuzungumza na wana CCM katika mikoa ambayo amepita.

Kabla ya Arusha na Kilimanjaro Kinana alianza ziara yake katika Mkoa wa Pwani na baadae mkoa wa Tanga.

Akizungumza mbele ya wana CCM Mkoa wa Arusha Kinaana amesema anawashukuru kwa mapokezi makubwa na mazuri waliyompatia.

“Nawapenda sana, baaa ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM nimeona nifanye amsha amsha kidogo, nimeanza ziara Mkoa wa Pwani, Tanga, Kilimanjaro na leo nimeingia hapa Arusha, nasema nimetia nanga na mengine tutazungumza kesho kwenye kikao kazi.Nawashukuru san asana.”

Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ambaye amekuwa akipata nafasi ya kusalimiana na wanachama wa Chama hicho na kubwa ambalo amekuwa akilisisitiza ni CCM kuendelea kushika dola.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...