NA MATUKIO DAIMA APP IRINGA

ASKOFU wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Blaston Gavile ametaka watanzania kuendelea kuliombea Taifa ili kuepuka machafuko ya kivita kama yanayoendelea kati ya Taifa la Ukrein na Urusi kwa kuwa madhara ya vita hiyo ni makubwa kwa binadamu kupoteza maisha na mali kuendelea kuharibiwa pia kuombea viongozi ili wawe na hofu ya Mungu katika kuongeza Taifa 

Askofu Gavile aliyasema hayo Leo wakati akitoa salamu za Pasaka kwa kanisa hilo kupitia waumini wa usharika wa kanisa kuu , alisema kuwa wakati waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Iringa wauaungana na kikristo kote ulimwenguni katika kusherekea sikukuu ya Pasaka kuna kila sababu kwa watanzania kumshukuru Mungu kwani nchi ina amani na utulivu wa kutosha .

" Wote tunafahamu kinachoendelea katika nchi nyingine mathalani vita ya Urusi dhidi ya Ukraine watu wanapoteza maisha na waathirika wakubwa ni watoto ,wazee na wanawake lakini tunaona namna ambavyo miundo mbinu inavyoharibika kutokana na silaha nzito ambazo majeshi yanatumia"

Alisema kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa (UN) watu zaidi ya 20,000 wamepoteza maisha na maelfu ya watu wanakimbia nchini humo kwa kukosa amani na utulivu pia gharama za maisha ikiwemo ya nishati ya mafuta ya imepanda duniani kote ambapo tunashuhudia bidhaa kama unga wa ngano ,mafuta ,huduma za usafirishaji zikipanda na kusababisha usumbufu kwa wananchi .

Askofu Gavile alisema jambo la msingi kwa waumini wa kanisa hilo ni kuomba Mungu aimalishe am,ani na utulivu ili watanzania wasiwe watu wa kulalamika au kushabikia mambo badala yake kuwa watu wa kufunga na kuombea amani na utulivu nchini izidi kuendelea kudumu kama ambavyo viongozi waasisi wakuu wa Taifa la Tanzania kama hayati baba wa Taifa Julius Nyerere Abeid Aman Karume walivyoweza kuacha amani na utulivu.

" Tuwaombee viongozi wetu kuanzia Rais Samia Suluhu Hassan ,makamu wa Rais Dkt Philip Mpango, waziri mkuu Kasim Majaliwa ,spika wa bunge Dkt Tulia Ackson na viongozi wengine ili Mungu awape afya njema ,hekima,busara katika kuongoza Taifa letu ili lifuate misingi ya utawala bora na kuleta maendeleo kwa Taifa"


HALI YA UKATILI KATIKA JAMII
Alisema kuwa kanisa ,jamii ,mashirika na wadau wengine kwa pamoja hakuna budi kushirikiana na serikali kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii .

Askofu Gavile alisema ripoti ya jeshi la polisi ya mwaka 2020 inabainisha ukatili wa ubakaji kwa watoto kwa kuwa na visa 7,263 vilivyoripotiwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 mwaka ambao viliripotiwa visa 5803 kwa hii ni ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi jambo ambalo linahatarisha mustakabali wa ustawi wa watoto .

"Kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko la matukio ya ukatili katika jamii yakiwemo ya ubakaji ,ulawiti wa watoto ,vipigo kwa wanawake na mauwaji ya kikatili kuwa Roho hii ya ukatili imeongezeka kutokana na watu kukosa upende na hofu ya Mungu kwa kutoheshimu na kuthamini uumbaji wa Mungu pia tamaa ya mali na imani za kishirikina ni miungoni mwa mambo yanayochangia kuongezeka kwa ukatili huu katika jamii"

Hata hivyo alipongeza idara ya familia na malezi KKKT Dayosisi ya Iringa kwa kuendelea kuzunguka katika sharika zote kufanya semina kwa watoto ,wazazi na walezi juu ya ukatili ,mafunzo ambayo yataamusha ari na uelewa wa kupinga vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea kinyume na mpango wa Mungu.

Pia aliomba waumini wote wa kanisa hilo wanaposherekea Pasaka kuingia katika toba ya kweli juu ya umwagaji damu zisizo na hatia nchini Ukrein kwani ni chukizo kwa Mungu pia kuomba kwa ajili ya vitendo vya ukatili vinavyoendelea nchini na kuombea Taifa amani .

MABADILIKO TABIA NCHI.

Alisema kuwa mabadiliko Taibanchi ni miongoni mwa changamoto kubwa inayoikumba dunia kwa sasa ambayo inasababisha kupungua kwa misitu ,mabadiliko ya utaratibu wa mvua na kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari kunaweza kuongeza shinikizo la kiuchumi ,kisiasa na kijamii lililopo na kuathiri maendeleo ya jamii .

Kuwa mwaka huu Taifa limeshuhudia mvua ikichelewa kuanza kunyesha na maeneo mengi hali inaonesha mazao mengi huenda yasikomae kwa kiwango sitahiki hali ambayo inaashiria huenda kukawa na upungufu wa chakula hivyo wakuu wa majimbo ,wachungaji na viongozi wengine wa kanisa na jamii wanapaswa kuelimisha wananchi kutunza chakula watakachovuna pia waliopo mabondeni ambako kuna ruhusiwa kulima basi wasisite kupanda mazao ya muda mufupi kwa ajili ya kukabiliana na hali hii ya hofu ya chakula.


SENSA YA WATU NA MAKAZI


Askofu Gavile alisema kuwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imepanga kufanya sensa ya watu na makazi ifikapo mwezi Agosti mwaka huu 2022 kuwa sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 wakati sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967,1978,1988 ,2002 na 2012.

" Zoezi hili liliasisiwa tangu enzi na enzi Tukisoma katika Biblia takatifu katika vitabu vya hesabu na Injili zote nne ( Luka ,Marko ,Mathayo na nyingine kuhesabu watu ni jambo la kawaida katika jamii yoyote ile yenye malengo chanya hata wana wa Israel pamoja na wazazi wa Yesu Kristo walihesabiwa hivyo kanisa tuendelee kuelimisha washarika wetu kushiriki zoezi la kuhesabiwa kwa ukamilifu muda utakapofika na kujiepusha na dhana ya upotoshaji kwani Sensa ni muhimu sana" alisema askofu Gavile .

Alisema sensa huisaidia serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025 ,mageuzi ya ,masuala ya afya na jamii ,pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa kwani taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamalaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa raslimali hivyo kila mmoja aendelee kuombea zoezi la sensa kufanyika kwa ufanisi zaidi .




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...