Na Jane Edward, Arusha

Jamii imetakiwa kutumia nishati ya biogas katika matumizi ya majumbani ili kuondokana na changamoto ya milipuko ya nishati ya gesi ambayo imekuwa ikileta madhara makubwa kwa jamii.

Hayo yamesemwa na mhandisi Nicolas Mwakisambwe kutoka kituo cha utafiti cha zana za kilimo Camartec wakati alipokuwa akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu.

Amesema kuwa biogas msingi wake mkubwa ni teknolojia ambayo inaenda zaidi kwa wakulima na wafugaji na inatokana na kinyesi cha wanyama pamoja na mimea ambapo husaidia kupata mwanga na kutumia nishati kwaajili ya kupikia.

Amebainisha kuwa familia nyingi za wafugaji maisha yao ni ya kuhama hama lakini pia uhaba wa maji ni changamoto kubwa kwakuwa wakati wa ujenzi wa biogas maji yanahitajika ya kutosha ili kukamilisha ujenzi huo.

Aidha amesema elimu kwa jamii ya kifugaji juu ya mtambo huo wa biogas ni ndogo kwa kuwa wengi wao hawajui faida na umuhimu wa nishati hiyo.

Amesema kuwa faida ya biogas ni usafi na kusaidia katika kilimo, kutunza mazingira na kutoa nishati ya mwanga kutokana na mtambo huo wa biogas.

"Teknolojia hii ni muhimu sana katika utunzaji wa mazingira tofauti na Kutumia Mkaa au kuni ambazo zinasababisha mtumiaji kupata madhara kutokana na moshi unaozalishwa na hivyo uwepo wa nishati mbadala ya biogas ni mkombozi na rafiki wa mazingira" Alisema

Aidha amesema kuwa wafugaji wengi hawajui matumizi ya kinyesi cha ng'ombe ambapo wakati mwingine hukitupa sehemu ambayo haifai na hivyo kusababisha mazingira kuwa machafu, harufu pamoja na mazalia ya wadudu ikiwemo Inzi.

Ameongeza kuwa wamekuwa na mradi wa kutengeneza mtambo wa nishati ya biogas kwa ngazi ya kaya na kwa nchi nzima wameweza kufundisha mafundi mia tano wa kujenga biogas ili kuweza kusaidia wananchi wanaotaka kujengewa mtambo huo.

Akizungumzia kuhusu mchango wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (COSTECH) katika mradi huo amesema wanapaswa kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ili kuweza kufikisha mbali zaidi biogas na kutumika na watu wengi hasa katika upande wa utunzaji wa mazingira.

Mtambo wa biogas ukitengenezwa.
Mtambo wa biogas ukiwa katika hatua za ukamilikaji.

Moto unaotokana na Nishati ya Biogas ambao unafaa kutumika kwa Kupikia.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...