Janeth Raphael - Dodoma

Serikali Imesema imetatua migogoro 18 kati ya 25 iliyopo.

Selemani Jafo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Muunganano wa Tanganyika na Zanzibar wamefanikiwa yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma.

Waziri Jafo amesema kuwa mwaka 2020 waliweza kutatua kero saba na kubaki kero 18 za muungano.

 “Lakini kwa uongozi wenu wewe (Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango) na mheshimiwa Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) tumefanikiwa kutatua kero 11 (mwaka 2021) na hivyo ukijumlisha na zile saba zinakuwa 18,”amesema.


Katika sherehe hizo  Makamu wa Rais Dkt  Philip Mpango  amezindua kitabu ambacho kinazungumza misingi ya muungano na maendeleo yake na kwamba kitabu hicho ni kitabu pekee tangu muungano ulipoanzishwa.

“Maelekezo yenu yamefanikisha hili, kitabu hichi kitakuwa ni nyenzo kwa Watanzania, nyenzo kwa wadau mbalimbali ya msingi, historia na maendeleo ya muungano katika miaka mbalimbali,” Waziri Jafo

Wakati huo huo Waziri Jafo amesema  kama itampendeza kinaweza kutumika katika somo la historia shuleni ili kupandikiza agenda ya ufahamu kuhusu muungano wa Tanzania na Tanganyika.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...