Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara ,Abdulrahman Kinana
amewapa onyo wagombea wa chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama
,wasitafute uongozi kwa Umaarufu wala fedha zao kwani kura hazinunuliwi.
Amezitaka kamati za siasa za mkoa,wilaya kutoona aibu wala Aya kuwakata majina wale watakaobainika kucheza rafu za rushwa.
Akizungumza
na wananchi na wanachama wa CCM Mkuranga,baada ya kutoka kuzindua
ujenzi wa tawi la Mwanambaya Kinana ,aliwataka wanachama waamue wenyewe
kuchagua viongozi bora na si Bora kiongozi.
Pia
alikemea mchezo wa kuchafuana ili mwingine ashindwe kugombea,na
kuongeza kamati za siasa zinataarifa za kina watu wasipotoshane na
kuchafuana.
"Kuchafuana
hapana, kubebana hapana,tafuteni uongozi kwa haki sio kutafuta viongozi
wako wa matawi,mashina kwa Ajili ya uchaguzi wa baadae"
"Siku
zote hawawatambui,huusalimii,huna habari nao, Uchaguzi ukifika ndio
unapitapita kutumia umaarufu, Kila mwanachama ana haki ya kugombea na
kuchagua na sio kununuliwa,":Mnakubaliana na Mimi";!
Kinana
alieleza, kabla ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti,aliitwa na
Rais,na baada ya kukubali,agizo la kwanza alilopewa ni kusimamia
uchaguzi kikamilifu.
"Mwenyekiti aliniambia nihakikishe uchaguzi unafanyika kwa Uhuru na haki,Nitasimamia hilo"
Vilevile
Kinana alibainisha kuwa, ukitaka uadilifu lazima CCM iwe mfano, Chama
hicho kimepewa ridhaa moja kuwa na sikilo la kusikiliza changamoto na
kero za wananchi ili zifikishwe sehemu husika.
"Wananchi
wanadhulumiwa tunanyamaza,tusinyamaze tuwasemee na tuna kazi kubwa ya
kusemea mazuri inayofanya Serikali ,nampongeza Mkuu wa mkoa wa Pwani
Abubakari Kunenge,Kaeleza yote yanayotekelezwa na Serikali na fedha
walizopokea kutoka Serikali na namna zilivyotumika:'"Naomba na
Anachoomba Rais kuungwa mkono,kupewa moyo"aliongeza Kinana.
Hakusita kuwapongeza wakurugenzi wa Halmashauri, viongozi wa matawi ,kata na madiwani na mabalozi ambao wanajitolea licha ya kufanya kazi kubwa .
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Saidi Goha Alieleza Mkoa una mashina
7,205 kati ya hayo 3,239 yameshafanya uchaguzi na 1,056 michakato
inaendelea ili kufanya uchaguzi.
Goha
alielezea kwamba Hali ya kisiasa Ni shwari, Utekelezaji wa ilani
unaendelea vizuri ikiwemo sekta ya elimu wanafunzi walikuwa wakisoma kwa
shida kutokana na uchache wa madarasa ,wananchi walichangishwa lakini
kufikia 2022 kadhia hii imeondoka .
Kwenye
vitega uchumi alisema ,lengo kumalizia ujenzi wa ukumbi Kama kitega
uchumi vya Chama na Sasa imefikia asilimia 75 ,mpango uliopo wamejipanga
kukopa fedha katika mfuko wa Chama ili ukumbi uweze kukamilika .
Alimshukuru
Kinana kwa kufika kufanya ziara Mkoani hapo ikiwa Ni mkoa wa kwanza
tangu achaguliwe na Ni siku ya 24 tangu achaguliwe.
Akitoa salamu za Serikali,mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge alisema ,2020-2025 inaendelea kutekeleza ilani ya CCM.
Akizungumzia
sekta ya elimu alisema, wanaendelea kuboresha miundombinu ya madarasa
ambapo Bilioni 17.1 zimetumika kujenga madarasa 108 ,huku Bilioni 8.4
zimetumika katika ujenzi wa Madarasa 422 ya Sekondari.
"Pia matundu ya vyoo 540 ,shule mpya 12 kwa Bilioni 5.64 ambazo zimeshatolewa
Katika
afya , Kunenge alieleza Kuna vituo vya afya 434 kimkoa na Kuna fedha
Jumla ya sh.bilioni 2.3 zilitolewa kupitia Tozo kwa Ajili ya ujenzi wa
vituo vya afya Tisa.
Kuhusu
Viwanda Kunenge, alinijinasibu mkoa huo ni ukanda wa viwanda na
unaongoza katika ambapo una viwanda 1,453 kati ya hivyo 87 Ni vikubwa .
Aliishukuru
kwa Serikali ya awamu ya sita kufungua miundombinu ya barabara
,ukiangalia bararaba ya Chalinze-Morogoro upembuzi yakinifu unaendelea
kwa Ajili ya kuendeleza upanuzi wa ujenzi ,pia Mlandizi -Mzenga-selous
ambapo jitihada zinaendelea na itakuwa barabara muhimu na ile ya
Madafu-mksigusugu km.12.5.
"Barabara
hizi zitasaidia kuleta Imani kwa wawekezaji kuona fursa ipo Mkoani
Pwani kwa kupunguza changamoto za Kero ya miundombinu korofi."Kunenge
alifafanua.
Sekta ya maji
, Kunenge alibainisha DAWASA imepokea Bilioni 228 kwa Ajili ya maji
kati ya hizo zinatekeleza miradi mikubwa kumi ambapo ikikamilika
itanufaisha Wakazi 834,000 na ile ya RUWASA ikikamilika itanufaisha
wakazi 99,334.
"Nawapongeza
Taasisi hizi kwani zimejipanga kufikia asilimia 95 kabla ya muda
uliolengwa na kupangwa ili kupunguza kero ya Ukosefu wa maji "alisema
Kunenge.
Kwa upande wake
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega alisema bado Kuna kazi kubwa
ya kufungua miundombinu ya barabara Vijijini , ikiwemo Mjini
Mkuranga-Kisiju katika bandari iliyojengwa toka enzi za ukoloni.
Alielezaa
bandari ile haifi na wanaomba awe balozi wakati akitaja bandari zote
asisite kuitaja ya Kisiju kwani inategemewa na wananchi Hadi wa Mafia.
Ulega
aliomba barabara ya Mkuranga-Kongowe ipanuliwe ili kupunguza ajali na
kusema , upo mradi mkubwa wa kimkakati Stendi ya mabus makubwa
wanatarajia kuuita Samia Suluhu Hassan na habari za matumaini kwa
wananchi ni kuwa mradi huo ukwenda kumalizika .
"Nakushukuru
kwa ziara hii kufanyika Mkuranga ,umetufanyia kazi kubwa na kuacha
Alama pale ulipofungua ujenzi wa tawi la Mwanambaya ambako Mimi
naishi"alisisitiza Ulega .
Alimshukuru
Rais kwa kazi aliyofanya mwaka mmoja kwa kutoa fedha nyingi za Uviko
kujenga madarasa pamoja na miundombinu ya barabara .
Mwenyekiti
wa CCM Pwani Ramadhani Maneno, Anaeleza juu ya Chalinze kuwa wilaya ,
amemuomba Kinana kuchukua nafasi kukaa na Mwenyekiti CCM Taifa kurejea
kauli ya Rais wa awamu ya tano marehemu John Magufuli aliyowaambia wana
Chalinze .
Maneno alisema Chalinze ni kubwa, vigezo vinazingatiwa japo igawanywe iwe ya kichama kama si Serikali.
Alimtoa
hofu mkuu wa mkoa wa Pwani,kumsaidia anapochukua Maamuzi mazito kwani
wapo baadhi wanachafua Serikali kwa mwamvuli na kisingizio cha chama.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akikagua jengo hilo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tawi la CCM Mwanambaya,Wilayani Mkuranga mkoani Pwani 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akifungua kitambaa ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tawi la CCM Mwanambaya wa Pili kushoto ni Mwenyekiti wa Shina hilo Bi Amina Ndomboroke
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akipanda mti mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tawi CCM Mwanambaya
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akmsikiliza Mwenyekiti wa Shina la CCM Mwanambaya Bi Amina Ndomboroke
Makamu Mwenyekiti wa wa CCM Tanzania Bara, Ndg Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka nmara baada kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tawi la CCM Mwanambaya
Makamu Mwenyekiti wa wa CCM Tanzania Bara, Ndg Abdulrahman Kinana akisalaimiana na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe.Abdalah Ullega mara baada ya kuwasilia kwenye ofisi za chama hicho Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Mkuranga katika Ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na WanaCCM Pamoja na Viongozi Mkoani Pwani.picha na MICHUZIJR-MMG.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...