Na Amiri Kilagalila
NAIBU
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu
Mwanaidi Ali Khamisi amesema kuna umuhimu mkubwa kwa watanzania
kujitokeza kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi kwa kuwa mbali
na faida zingine pia itasaidia kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa
kijinsia nchini.
Ametoa
rai wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kuwa kufanya hivyo kunasaidia
kuunga mkono juhudi zinazofaanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuiletea
nchi maendeleo.
Akizungumza
na baadhi ya vyombo vya habari Mwanaidi alisema ni muhimu kwa kila
mtanzania kushiriki kikamilifu katika mchakato huo ili kusaidia ukuaji
wa maendeleo ya nchi kama ambavyo Rais Samia amesisitiza.
"Sensa
ni muhimu, hauwezi kupanga maendeleo ya nchi kama hujajua idadi ya watu
ulionao, Rais amesisitiza kuwa sote ni vyema tukajitokeza na kushiriki
katika zoezi hilo Agosti 23 Mwaka huu, niwasihi tusimwangushe,
tujitokeza kikamilifu" alisema Mwanaidi
Amesema
kama Taifa kuna manufaa mengi ya kushiriki sensa hiyo, hivyo ni vyema
kila mtu akaona umuhimu wake na kujitokeza siku hiyo kufanikisha suala
hilo litakalotusaidia watanzania katika kujiletea maendeleo.
Mbali
na hilo Mwanaidi pia alisema kwa kujitokeza kushiriki Sensa hiyo,
kimsingi kutaiwesha Serikali hususani Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Waanawake na Makundi Maalumu kutoa elimu ya ukatili kijinsia
uliopo katika nchini kwa urahisi na kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo.
Awali
akizindua nembo ya sensa hiyo sambamba na tarehe ya kufanyika kwake,
Rais Samia Suluhu Hassan alisesema zoezi hilo i muhimu kwa kuwa
litaisaidia Serikali kuandaa sera na mipango mipya ya maendeleo ya muda
mfupi na muda mrefu na jinsi ya kuitekeleza na kufatilia utekelezaji wa
mipango hiyo.
Alisema
taarifa hizo zitakazopatikana kupitia zoezi hilo pia zitasaidia kujua
wastani wa ongezeko la watu na hali ya uhamiaji mfano kutoka vijijini
kuja mjini lakini hata waliotoka nje kuhamia na kuingia Tanzania.
"Sensa
pia itatusaidia Serikali kufanya maamuzi kuhusu ugawaji wa rasilimali
za Taifa na kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo afya, elimu,
maji, umeme, ujenzi wa miundombinu kulingana na idadi ya watu na
mahitaji ya maeneo hayo" alisema Rais Samia.
“Ili
Sensa iweze kukidhi mahitaji ya kufanikisha malengo yote hayo ni lazima
ishirikishe watu wote. Zoezi hili litakuwa ni kwa watu wote waliolala
na kuamkia siku ya Sensa kwenye nchi ya Tanzania,” alisema Rais Samia.
Alisema
licha ya uwepo wa tozo za makazi, Serikali haikuwa na idadi sahihi ya
nyumba na makazi, hivyo zoezi hilo litatoa ubora kwa kujua anuani za
makazi, idadi ya majumba na aina za nyumba zilizopo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...