Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, anayehudumu kama fundi maji wa Mamlaka ya Maji Safi DAWASCO, Tawi la Kimara, Ally Kayuni, amefanikiwa kuibuka na dodo la Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa ya bahati nasibu ya biko, iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kayuni alisema ameshinda baada ya kucheza kwa kuingia www.biko.co.tz na wakati mwingine kutumia mfumo wa namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 jambo lililomfanya atangazwe kama mshindi wa biko..

Alisema Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wamekuwa kuanzia sh 2500 hadi Milioni 5 papo kwa hapo pamoja na droo kubwa za kila Jumapili.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.
Balozi wa Biko, Kajala Masanja kushoto, akimkabishi fedha zake mshindi wao wa sh Milioni 10, Ally Kayuni mwenye makazi yake Kimara, jijini Dar es Salaam katikati. Mwingine kulia ni Janeth Msuya, Meneja wa Uhusiano wa CRDB, Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu.


Mkazi wa Kimara, Ally Kayuni akiwa na shangwe kubwa wakati anakabidhiwa fedha zake sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Anayemkabidhi ni Janeth Msuya, Meneja Uhusiano wa Bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu.Mkazi wa Kimara, Ally Kayuni akiwa na shangwe kubwa wakati anakabidhiwa fedha zake sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Anayemkabidhi ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...