Na John Walter-Manyara
Mbunge wa Vijana Taifa kutoka
mkoa wa Manyara Asia Halamga ametoa msaada wa Karatasi (REEM PAPERS) kwa
ajili ya uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye majimbo yote
Matano ya mkoa wa Manyara.
Halamga
amekabidhi Karatasi hizo leo Mbele ya Katibu wa NEC, Siasa, Itikadi na
uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka Katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi
mjini Babati.
Amesema
Karatasi hizo zitasaidia katika zoezi la kutoa fomu za kugombea nafasi
mbalimbali na kuondoa usumbufu wa kusuasua kwa utoaji wa fomu hizo
katika majimbo ya mkoa wa Manyara.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Babati Daniel Muhina amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo akieleza kuwa ametoa katika muda muafaka ambao Chama kinaendelea na chaguzi zake ndani ya Chama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...