Na Bakari Madjeshi,Michuzi TV
BAADA ya Klabu ya Simba kutoa taarifa ya kumpa mapumziko mchezaji wake mahiri Bernard Morrson hadi mwisho wa msimu, mchezaji huyo amesema anatamani kueleza mengi kuhusu suala hilo lakini ameamua akaae kimya.
Morrison ambaye ni raia wa nchini Ghana aliungana na Klabu ya Simba baada ya kutokea timu ya soka ya Yanga na alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.
Baada ya Simba kutangaza makubaliano yaliyofikiwa kati yao na Morrison , mwenyewe amesema hivi “Ni ngumu kusema, kuwa nje ya timu hadi mwisho wa msimu huu wa mashindano, kutokana na masuala ya kifamilia ambayo yanakwamisha kiwango chake ndani ya Klabu hiyo.
“Nahitaji kusema mengi kuhusu hili suala, lakini naitakia kila la kheri Klabu katika michezo yake iliyobaki, naamini nitapata suluhisho la masuala yangu haraka iwezekanavyo na kujiunga na timu hapo baadae”, ameeleza Morrison kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Awali kabla ya Morrison kutoa kauli hiyo, Simba kupitia Ofisa Mtendaji mkuu wa Klabu hiyo Barbra Gonzalez katika taarifa yake kwa umma amesema
wamempa mapumziko hadi mwisho wa msimu Morrison baada ya makubaliano ya pande zote mbili, ili kumpa nafasi Mchezaji huyo kushughulikia mambo yake binafsi.
Klabu hiyo mapema leo imeeleza kumshukuru Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alipokuwa akitumikia Klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi, jijini Dar es Salaam.
“Tunatambua na kuthamini mchango wa Bernard Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia Klabu yetu na kusaidia kupata mafanikio kadhaa ikiwemo kucheza Robo Fainali ya Michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC) na Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi”, imeeleza Taarifa hiyo.
Pia, taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa mchango na mafanikio hayo Klabu inamshukuru Mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba SC kwa kujitoa kwake katika kupigania Klabu hiyo, Simba SC imemtakia kila la kheri Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya Soka hapo baadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...