Na Mashaka Mhando, Muheza
KIONGOZI
wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2022, Sahil Geraruma, amezitaka kamati
zinazosimamia miradi mbalimbali nchini kuhakikisha wanafuata taratibu za
za kifedha ili miradi inayotekelezwa isiwe na kasoro.
Akizungumza
katika mradi wa kwanza tangu aingie wilayani Muheza kutokea wilayani
Mkinga, Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2022 alisema serikali
ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha
kugharamia miradi mbalimbali hivyo ni vema ikasimamiwa vizuri.
Alisema
hayo baada ya kukagua nyaraka za mradi wa nyumba nne za shule ya
sekondari Misozwe pamoja na nyumba ya mganga Mkuu wa hospitali ya
wilaya ambapo alizikuta kasoro katika sehemu za utiaji wa sahihi
unaopaswa kuwekwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo imewekwa na mtu
mwingine.
"Mradi
huu ni mzuri mmejitahidi na hongereni kwa kuutekeleza japo kuna dosari
ndogo ndogo za nyaraka za malipo zipo tofauti kati vipengele,"
"Viongozi
mnaopewa dhamana ya kusimamia miradi fuateni taratibu mnajisahau hasa
katika suala la nyaraka za malipo, ubora wa majengo tunautazama hata
katika nyaraka za malipo," alisema.
Akiwasilisha
ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka huu, kiongozi huyo aliwataka wananchi
wajitokeze katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti
23 mwaka huu, kwa ajili ya muskabali wa Maendeleo ya nchi.
Awali
akiupokea mwenge huo Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akiwa na
mbunge wa jimbo hilo Hamisi Mwinjuma almaarufu MwanaFA, alisema Mwenge
wa Uhuru utatembelea miradi ya Maendeleo ipatayo nane katika sekta ya
afya, elimu na maendeleo ya jamii yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7.
Mkuu wa wilaya alisema katika miradi hiyo miwili itazinduliwa na miwili kuwekewa mawe ya msingi na miradi mingine minne itaonwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya Muheza Nassib Mmbaga alisema miradi
iliopitiwa na Mwenge ni pomoja na mwenge kupokea taarifa za zoezi la
anuani za makazi na maandalizi ya uhamasishaji na utoaji wa elimu ya
sensa ya watu na makazi kwa jamii katika kijiji cha Kicheba.
Alisema
pia mwenge umekabidhi meza, viti na makabati kwa ajili ya wanafunzi
wenye mahitaji maalumu, samani zilizotengenezwa na fedha za Mwenge.
Pia
Mkurugenzi huyo alisema mwenge ulipokuwa Muheza umeweza kufungua mradi
wa vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa kwa fedha za Uviko-19 na
vyumba 4 vilivyomaliziwa na fedha zilizopatikana kutokana na fedha za
tozo na fedha za serikali katika eneo la kata ya Genge.
Akizungumza
katika mradi wa uwezeshaji kiuchumi kwa vijana wa usindikaji wa mkonge
katika kitongoji cha Masimbani kilichopo kata ya Kwemkabala, mbunge wa
Muheza MwanaFA aliwapongeza vijana katika mradi huo aliosema
umemfurahisha kwa vile umelenga kuwaondoa katika umasikini.
Alisema
mwenge unapopita kukagua na kuzindua miradi unasaidia kuhakikisha fedha
zilizotolewa na serikali zinatumika vizuri katika miradi ya maendeleo.
"Mradi
huu ni mzuri na nineupenda, hawa akina mama na baba wakifanya vizuri
katika mradi huu watakuwa mamilionea," alisema MwanaFA.
Miradi yote minane imefunguliwa na kuwekewa mawe ya maingi na mingine ilionwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2022 Sahil Geraruma akizungumza na wananchi wilayani Muheza
wa Muheza Mhe Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA akiwapungia wananchi mkono
Mbunge wa Muheza Mhe Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA akiwa ameushika mwenge wa Uhuru baada ya kuanza mbio katika wilaya hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Mkinga Col.Maulid Surumbu akimkabidhi mwenge wa Uhuru mkuu
wa mkoa wa Muheza Halima Bulembo ili aukimbize katika wilaya hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...