Na Pamela Mollel,Arusha
Kituo cha Sheria na haki za Binadamu(LHRC) imetoa taarifa ya Matukio ya Ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini huku ikitaja mikoa ya Arusha,Dar es Salaam,Shinyanga,Tanga,Mwanza na Dodoma ikiongoza kwa matukio hayo
Akizungumza katika mkutano jijini Arusha Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Fulgence Masawe alisema ndani ya miaka miwili, 2020 na 2021 ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto yameongezeka
Alitaja takwimu za mwaka 2020 zinaonesha kuwa makosa ya ukatili wa kijinsia dhidi ya mwanamke majumbani yanayotokana na wivu wa mapenzi na yaliyoripotiwa yalikuwa 41,673 huku Mwaka 2021 yakishuka na kufikia 29,000.
Aliongeza kuwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto mwaka 2020 yalikuwa 15899 na mwaka 2021 yalifikia 11499 .
Aidha alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 kituo cha LHRC kimepokea ripoti ya matukio ya mauaji ya mwanamke 30 ambayo yametoka na ukatili wa majumbani unaotokana na wivu wa mapenzi.
Alisema kuwa suala la ukeketaji ni sehemu ya matukio ya ukatili ambayo yamekuwa yakiongezeka katika mikoa ya Arusha,Tanga,shinyanga ,Mwanza na Ilala.
Alisema hatua hiyo imelazimu LHRC kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa ustawi wa jamii katika mikoa yote nchini ispokuwa Manyara na Dae es salaam.
"Mwaka huu tumeonelea tuwajengee uwezo waendesha mashtaka wa serikali na mawakili ili wanapofanya kazi zao wajue namna ya kutenda haki katika kulinda na kusimamia misingi ya haki za binadamu"alisema.
Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa waendesha mashtaka katika kulinda kutetea na kusimamia maslahi ya wanawake na watoto pamoja na watu wenye ulemavu,kituo kimeungana na wizara ya katiba na sheria kuwajengea uwezo waendesha mashtaka takribani 100
Naye Mkurugenzi wa mashtaka nchini DPP,Sylvester Mwakitalu aliwataka waendesha mashtaka kusimamia vema haki wakati wakiendesha mashauri ya kijinsia mahakamani na kuleta matokeo chanya na yenye tija .
Alisema tatizo la ukatili kwa mwanamke na watoto bado ni kubwa sana hapa nchini kuliko takwimu zinazotajwa kwa sababu mengi hayatolewi taarifa katika vituo vya polisi hivyo kwa waendesha mahistaka kunahitaji umahili na weredi mkubwa.
"Mimi nitafuatilia kwa waendesha mashtaka mmoja mmoja na nitafika kila mkoa na wilaya ili kuona waendesha mashtaka mnavyosimamia mashauri hayo ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto"alisema
Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya sheria na katiba Mary Makondo alisema wizara ya katiba na sheria inajukumu kubwa la kusimamia mfumo mzima wa haki jinai nchini katika kufanya marekebisho ya sheria na sera zinazosimamia mfumo huo .
Alimtaka mwendesha mashtaka wa serikali kuzidisha kutoa fursa za kuwapatia mafunzo zaidi na wajibu , waendesha mashtaka nchini ili kuwajengea uwezo waweze kutenda majukumu yao kwa haki na weredi mkubwa.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia namna ya kutatua changamoto mbalimbali za kisheria inayopelekea ucheleweshaji na uendeshaji wa mashauri ili kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani na msongamano wa mahabusu magerezani.
Mkurugenzi wa mashtaka nchini DPP, Silvester Mwakitalu
Katibu mkuu wizara ya sheria akizungumza katika mkutano jijini Arusha
Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Fulgence Masawe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...