Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
Raia wa Ufaransa na Mawakili wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kughushi nyaraka za nguvu ya kisheria.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Kija Elias mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mhina wametajwa hao ni, Bernad Bougault raia wa Ufaransa, Resb picious Mukandala na Simphorian Kitare ambao ni mawakili wa kujitegemea.
Akisoma hati ya mashtaka Kija amedai Februari 18, 2020 katika mtaa wa Samora washtakiwa hao walifoji nyaraka zilizoonesha kuwa Kapteni Phillipe Gerniers amemchagua Boulgault kuwa mwakilishi wake kisheria na wakala wake.
Katika hati hiyo inaonyesha Gerniers amempa Boulgault Mamlaka ya kufungua mashtaka kwa ajili ya mali zake zilizoko katika Hoteli ya Bagamoyo Beach au alipwe kiasi cha ASD 80,000 kwa niaba yake huku wakijua nyaraka hizo so za kweli.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na wameiomba mahakama kutoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa kwa kuwa kosa linalowakabili linadhamana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 23, 2022 kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamepelekwa mahabusu Baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kuwa na mdhamini mmoja kila mmoja mwenye barua ya utambulisho sambamba na kulipa kiasi cha USD 40,000 au kuepeleka hati ya mali isiyoyamishika yenye thamani hiyo ya pesa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...