Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MWANAMITINDO wa kimataifa Millen Happiness Magese amesema filamu ya The Royal Tour ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki kama mhusika mkuu inakwenda kufungua fursa mbalimbali ikiwemo ya uchumi na utalii huku akieleza kuna kila sababu ya Watanzania kumpongeza Rais kwa uthubutu wake.

Akizungumza na Michuzi TV Mei 8,2022 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Filamu ya The Royal Tour , mwanamitindo huyo ambaye amejizolea sifa katika mataifa mbalimbali duniani amesema tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo nchini Marekani amekuwa akiifuatilia kwa karibu sana na amelazimika kusafiri kutoka Marekani kuja nchini ili kushuhudia uzinduzi huo.

“Nafuatilia kwa karibu sana hili ni jambo kubwa kwa watanzania nan chi nzima kwa ujumla, nafikiri sisi kama watanzania kwanza tumpongeze mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan , Filamu hii inakwenda kuitangaza nchi yetu duniani.Jana nimeangalia uzinduzi wa The Royal Tour kule Zanzibar na nimeona kuna jambo kubwa la  kihistoria marais wetu wawili wameshiriki.

“Ni jambo la  kujivunia na tuko tayari na sisi tulioko nje ya Tanzania tunayo nafasi ya kuelezea Royal Tour kwa ukubwa unaostahili, hivyo nitoe rai kwa watu wote mashuhuri na maarufu  waiongelee filamu,”amesema Millen ambaye amelazimika kusafiri kutoka nchini Marekani kwa ajili ya kuja Tanzania kushuhudia uzinduzi wa filamu hiyo.

 Aidha amesema baada ya kuzinduliwa kwa The Royal Tour anaiona jinsi ambavyo Tanzania inakwenda mbali zaidi hasa katika kutangaza utalii uliopo pamoja na fursa nyingine za uwekezaji.”Filamu hii inasaidia kuonesha utajiri tuliona. Roya Tour inakwenda kunyanyua sekta zote na filamu hii  imesimama kama tangazo.

“Hivyo  watalii na wadau wa sekta nyingine watatamani kuja kuwekeza nchini, sekta nyingi ambazo ziko kwenye uchumi na burudani zitakwenda kunyanyuka, hakika Mama yetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakupenda.”

Aidha amesema katika kila jambo lazima wapo watakaokubali na watakaopinga,hakuna jambo ambalo linaweza kukubalika kwa asilimia 100, hivyo hashangai kuona baadhi ya watu wachache wakikosoa lakini jambo la faraja Watanzania wengi wanapongeza.

“Siku zote imekuwa hasini kwa hamsini, kikubwa ambacho tunakiangalia mama amepata uthubutu wa kufanya filamu hii.Uthubutu wake unakwenda kuifanya Tanzania kutambulika duniani na sehemu kubwa hii filamu inakwenda kuitangza nchini katika sekta mbalimbali.”
MWANAMITINDO wa kimataifa Millen Happiness Magese alipokuwa akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwenye hafla ya kushuhudia uzinduzi wa Kitaifa  wa Filamu ya The Royal Tour ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki kama mhusika mkuu,iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere Mei 8,2022 jijini Dar es Salamu.Picha na Michuzi JR-MMGMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...