MSHINDI wa pili Miss Utalii Tanzania 2021, Judith Ngusa, usiku wa kuamkia leo, ameibuka mshindi wa kwanza katika fainali za dunia za Miss United Nations 2022, zilizo fanyika New Delhi India.
Judith anakuwa mrembo wa kwanza Tanzania , kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya dunia, ikiwa ni mwendelezo wa rekodi shindano la Miss Utalii Tanzania kushinda taji katika mashindano yote tuliyo wakilisha Tanzania. Kwa ushindi huo kuendeleza rekodi yetu ya kushinda mataji katika fainali za dunia, Judith Peter Ngusa, anakuwa ni Mrembo wa Saba wa Miss Utalii Tanzania kushinda mataji mbalimbali katika fainali za dunia,
BAADHI ya walio wahi kushinda ni Ritha Sipilian - Miss Tourism world 2007 - Africa,Killy Janga - Miss Tourism World 2006, SADEC, Witness Manwingi - Miss Tourism World 2005.
Judith Ngusa : age 23, height 173 cm, Academic Bachelor Degree in Chinese Language, other profession cabin Crew and flight Safety Officer.
Other Title: Miss Tourism Lindi,Miss Tourism Eastern Zone and 1st Runner Up Miss Tourism Tanzania 2022
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...