Na Amiri Kilagalila,Njombe
Serikali
ya mkoa wa Njombe imezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa
polio awamu ya pili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano zoezi
ambalo litafanyika kwa siku nne.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ameongoza zoezi hilo kwa kutoa chanjo
kwa watoto kwa ushirikiano na wataalamu wa afya katika kituo cha afya
cha Njombe mjini na kubainisha kuwa katika awamu ya pili tena watoto
zaidi ya laki moja na kumi wanatarajia kupata chanjo hiyo.
“Ni muhimu kulinda na kukinga watoto wetu kwa kuwa hii ndio Tanzania ijayo,tunatakiwa kuwalinda watoto wetu”alisema Kindamba
Vile
vile Waziri Kindamba amewapongeza na kutoa zawadi kwa wanaume
waliojitokeza kufikisha watoto walio chini ya umri wa miaka mitano
kupata chanjo ya ugonjwa wa Polio kwa njia ya matone.
“Wababa
kama hawa wamebaki wachache sana,baba ambaye anamsindikiza mama ili
mtoto apate chanjo,sina shaka baba wa namna hii hata mama alipokuwa
mjamzito alikuwa anaambatana naye kwenda Kliniki”alisema Kindamba
Kindamba
amesema katika awamu ya kwanza mkoa wa Njombe umevuka lengo kwa
kuchanja watoto kwa 116% huku akibainisha kuwa zoezi hilo linaendelea
kwa mikoa minne ya Njombe,Mbeya,Ruvuma na Songwe ambayo ipo jirani zaidi
na nchi ya Malawi ulikoanza kuibuka ugonjwa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...