Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka
Hamdu Shaka, amewataka viongozi mbalimbali wanaofanya ziara hususan
katika miradi ya maendeleo kuwapa fursa wananchi kuona kinachofanywa na
serikali.
Shaka
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipotembelea soko Kuu la
Kariakoo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM, likiwemo Soko la Kariakoo alikoshuhudia hatua nzuri za
ukarabatibwake.
"Ndugu
zangu viongozi nadhani sasa ni muda mwafaka kubadilika katika hizi
ziara, badala ya kukaa na kujifungia na kuzungumza sisi wenyewe, ni
vyema tukawapa nafasi wananchi kuona Yale yanayofanywa na serikali yao
chini ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema.
Shaka
ameipongeza serikali kwa kazi nzuri inayofanya katika ujenzi
nabukarabati wa soko hilo ambapo amesema litakapokamilika manufaa yake
hayatakuwa kwa Kariakoo pekee bali ni kwa Dar es Salaam na Afrika
Mashariki yote.
Awali
akimkaribisha Shaka, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ludigija
Ng'wilabuzu, aliwapongeza wakandarasi wa mradi huo kwa kuutekeleza kwa
kasi.
Amesema
mradi huo upo chini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo amesema
kazi inaendelea vizuri na anaamini itakamilishwa katika muda muda wa
makubaliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...