Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma wakiwa kwenye mazungumzo na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann waliofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo namna ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kupitia mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani. (Picha na Edward Kondela – Afisa habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah akisoma moja ya nyaraka za mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kuanzia Mwezi Agosti Mwaka huu katika kipindi cha miaka minne kwa thamani ya Euro Milioni 2.17 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.2, mradi utakaotekelezwa Kaskazini mwa Tanzania katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kwale Mkoani Kenya, mara baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Tamatamah amesema mradi huo una faida kubwa katika kuhifadhi bainuai na kutoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo. (Picha na Edward Kondela – Afisa habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei akichangia hoja wakati wa mazungumzo baina ya ujumbe wa Tanzania kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini pamoja na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) juu ya mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kuanzia Mwezi Agosti mwaka huu. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam. (Picha na Edward Kondela – Afisa habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Kutoka kushoto ni Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma wakimsikiliza Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann waliofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam kuzungumzia mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani, utakaofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani katika kipindi cha miaka minne. (Picha na Edward Kondela – Afisa Habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann (kulia kwake) na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel (kushoto kwake), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) (wa kwanza kushoto) na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila (wa kwanza kulia), mara baada ya kuhitimisha mazungumzo ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani hususan katika Sekta ya Uvuvi yaliyofanyika katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam. (Picha na Edward Kondela – Afisa Habari, Wizara ya Mifugo na Uvuvi)Na. Edward KondelaKatibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amekutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kufanya mazungumzo ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kwenye uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.

Akizungumza leo (13.05.2022) mara baada ya kukutana na ujumbe huo katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam, Dkt. Tamatamah amesema katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kutakuwa na miradi mingi ambapo kwa kuanzia Mwezi Agosti Mwaka huu 2022, mradi utafanyika Kaskazini mwa Tanzania katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kwale Mkoani Kenya.

Katibu mkuu huyo mara baada ya kukutana na ujumbe huo ambao ni Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema Tanzania itapata Euro Milioni 2.17 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.2 kwenye mradi huo katika kipindi cha miaka minne.

“Huu mradi una faida unalenga kuhifadhi bainuai, utatoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo na tunategemea mradi utafanya rasilimali kuwa endelevu kwa muda mrefu na utaongeza kipato kwa wananchi, kwa kuwa wataelimishwa njia mbadala za maisha na kuhifadhi Maeneo Tengefu.” Amesema Dkt. Tamatamah.

Naye Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema ana furaha kwamba ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania katika maeneo ya bainuani na Maeneo Tengefu utakuwa na nguvu katika kuhakikisha Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi unatunzwa pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo katika Maeneo Tengefu zinaendelezwa, huku Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema mradi huo utajenga uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo baina ya Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann pamoja na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma ambapo mradi huo utatekelezwa na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...