Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Productions,Rita Paulsen maarufu kwa jina la Madame Rita amesema filamu ya The Royal Tour imetengenezwa kwa ustadi mkubwa na jambo ambalo amevutiwa nalo ni namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan ambavyo ameuvaa uhusika.

Akizungumza na Michuzi TV saa chache kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kuizindua filamu ya The Royal Tour jijini Dar es Salaam ,Madame Rita amesema anampongeza Rais Samia Samia kwa kuuvaa uhusika na kushiriki katika filamu ambayo haijawahi kufanywa hapa nchini Tanzania.

“Kwa hiyo hii filamu italeta hamasa kubwa sana kwasababu Rais aliigiza vizuri , alivaa vizuri , kulikuwa na uhalisia sana, nampongeza Rais wetu.Nimeona, vipande vichache lakini nachoweza kusema imetengezwa kwa ustadi mkubwa sana.”

Madame Rita ambaye kwa miaka kadhaa sasa kupitia kampuni yake amekuwa akiibua vipaji vya wasanii wa muziki, amesema filamu ya RoyalTour imethibitisha kwa vitendo wanawake wanaouthubutu wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya Taifa lao.”Rais Samia amethibitisha kuwa wanawake wanaweza hata yale ambayo wengine wanaamini hayawezekani.Ameonesha uthubutu na uzalendo mkubwa kwa nchi yetu.”


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...