




Akitoa maoni yake kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema, “Kupitia ubunifu na bidhaa zetu za hivi punde, lengo letu ni kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha bora na rahisi zaidi. Huu ukiwa ni mwezi wa Eid al-Fitr, tunatoa nafasi kubwa kwa kila mtu kuchagua maisha haya bora sio tu ya leo bali ya kesho pia”. "Hii pia ni fursa kwa Watanzania kubadilisha na kuboresha burudani zao za nyumbani au vifaa ambavyo wamekuwa navyo kwa muda mrefu hadi kufikia teknolojia mpya, ya kisasa na vifaa vya ufanisi zaidi".
Hii si tu katika maduka yenye chapa ya LG bali pia katika maduka makubwa ya washirika kama vile Shoppers na Game Super Market. Wanunuzi wamehakikishiwa kupata punguzo kubwa la hadi Tsh 539,200/=kwenye jokofu za LG Instaview 668(L), na Tsh 225,000/= kwenye jokofu la LG Instaview 544(L). Kwenye mashine za kufulia zinazotolewa, punguzo linaanzia Tsh 100,000/= hadi Tsh. 300,000 kwa mashine za kufulia ya 8Kg hadi ya 15Kg / dryer. LG microwaves, Neo Chef 20L, 23LNeoChef na 42L Neo Chef zote zina punguzo la kati ya Tsh 81,600/= na TZsh 122,800/= Kufahamu zaidi kuhusu kampeni hii kabambe tafadhari tembelea mitandao ya kijamii ya LGs East Africa. 

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...