Wizara imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, ikiwa ni pamoja huduma kabla ya kujifungua, Wakati wa ujauzito, Wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.

Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, kwa upande wa
huduma kabla ya ujauzito Wizara kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ilinunua na kusambaza vidonge vya uzazi wa mpango dozi 1,755,349 sawa na asilimia 82 ya lengo, sindano za uzazi wa mpango aina ya depoprovera dozi 2,125,625 sawa na asilimia 93 ya lengo na vipandikizi 206,000 sawa na asilimia 78 ya lengo. Katika kipindi hicho, wateja waliotumia njia za uzazi wa mpango walikuwa 4,189,787 ukilinganisha na wateja 4,357,151 wa mwaka 2020.

“Idadi ya wateja waliopatiwa huduma za uzazi wa mpango imepungua kutokana uwepo wa mlipuko wa UVIKO.” Amesema Waziri Ummy

Aidha Wizara imeendelea kuimarisha upatikanaji wa
huduma za afya wakati wa ujauzito (Antenatal Care) ambapo inakadiriwa kuwa kila mwaka akinamama wapatao milioni 2.3 hutarajiwa kupata ujauzito nchini.

“Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, jumla ya Wanawake wajawazito 1,784,809 walihudhuria Kliniki na
kupatiwa huduma za Afya na kati yao, asilimia 99.7 ya akinamama
wajawazito walifanya mahudhurio manne au zaidi ikilinganishwa na
asilimia 85 mwaka 2020.” Amesema Waziri Ummy

Hata hivyo changamoto iliyopo ni wanawake wajawazito kuchelewa kuhudhuria klinik wapatapo ujauzito huku Takwimu
zikionesha kuwa kati ya wajawazito 1,784,809 ni wajawazito 656,040
sawa na asilimia 37.6 walianza kupata huduma za wajawazito chini ya wiki 12 za mwanzo wa ujauzito, ikilinganishwa na asilimia 36 ya kipindi kama hiki mwaka 2020.

“Nitumie Bunge lako tukufu kuhimiza wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ndani ya wiki 12 za mwanzo wa ujauzito na kukamilisha mahudhurio yote 8 ili kuepuka kupata changamoto mbalimbali zinazoweza kusababisha vifo vyao na vichanga vyao wakati wa kujifungua.” Amesema Waziri Ummy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...