Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekabidhi gawio lenye thamani ya Shilingi bilioni 11.85 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF CPA Hosea Kashimba kwa niaba ya Mfuko, kwenye hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Akikabidhi hundi hiyo Mhe. Mchemba amesema, "nimefurahishwa pia kuona taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali, Halmashauri, pamoja na vyama vya ushirika wanapokea gawio la jumla ya Shilingi bilioni 16.4. Hii inafanya jumla kuu ya gawio tunalolipokea leo kuwa Shilingi bilioni 36.1. Ni jambo la kujivunia sana kwa Benki yetu ya kizalendo".




Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba

Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi (wakwanza kushoto) akiungana na maafisa wengine kwenye hafla ya kupokea gawio kutoka benki ya CRDB jijini Dodoma Juni 29, 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...