Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV


WIZARA ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imesema ripoti ya utafiti wa nafaka hasa eneo la usindikaji vyakula iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) itasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zipo katika sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa ripoti hiyo Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, ameeleza kwamba wanaamini kupitia ripoti hiyo ya WFP itasaidia kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo hasa katika uchakataji wa nataka unaofanywa nchini Tanzania.

"Ripoti hii ambayo tumeizindua  itasaidia Serikali kubaini maeneo yenye changamoto na kutatua kwa faida ya wachakataji wa nafaka na Serikali Kwa ujumla wake.Lengo la Serikali ni pamoja na kusimamia ubora wa Viwanda nchini Kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo(SIDO) ili kusaidia wazalishaji na wasindikaji waendelee kuweka virutubisho kwenye uzalishaji wao."

 Amefafanua kuwa ni vema SIDO ikatenga  maeneo tofauti yenye mazingira mazuri kwa wachakataji wa bidhaa za nafaka ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

Akielezea ripoti hiyo ya utafiti Mwakilishi Mkazi na Mkurugenzi wa WFP Tanzania, Sarah Gordon-Gibson amesema imebainika katika Viwanda 33,000 vya usindikaji vyakula, asilimia 90 haviweki virutubisho.

"Utafiti huu ulienda sambamba na Sensa ya wamikiki wa Viwanda vya kusindika vyakula pamoja na kujua uwepo wa virutubisho.Utafiti ulilenga hasa kujua idadi ya viwanda, mahali vilipo, aina ya mashine zinazotumika na uwezo wake,pia kubaini uwepo wa virutubisho, ripoti inaonyesha viwanda vingi haviweki virutubisho," amesema Sarah.

Pamoja nahayo amesema WFP wanatoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwani imesaidia kupatikana takwimu kwenye utafiti huo na kuahidi wataendelea kushirikiana ili kuiinua  sekta hiyo ya usindikaji wa nafaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...