Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es salaam na Pwani, Brigitta Shirima (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania PLC, George Lugata wakikata utepe kuzindua rasmi banda la kampuni ya Vodacom Tanzania Plc kwenye maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara sabasaba jijini Dar es salaam, ambapo mwaka huu kutakuwa na ofa na huduma mbalimbali ikiwemo punguzo la asilimia 10 kwa wateja wanaolipa kwa huduma ya lipa kwa simu. Kulia ni mtoa huduma wa kampuni hiyo Sarah Stephen


Kampuni ya teknolojia na Mawasiliano nchini Vodacom Tanzania Plc, Leo imezindua rasmi banda lake kwenye maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara (sabasaba) jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mkuu wa Mauzo wa kanda ya Dar es salaam na Pwani, Brigitta Shirima alisema, “Mwaka huu Vodacom tumekuja kivingine ambapo tunatoa wigo mpana wa huduma mbalimbali kwenye maonesho haya ili kuwapa wateja wetu na watanzania kwa ujumla waweze kufurahia huduma zetu, tuna huduma ya 4G ya kweli na punguzo kubwa la asilimia 10 % kama mteja atanunua simujanja kwa njia ya lipa kwa simu.

Tuna huduma kwa jamii kupitia asasi yetu ya Vodacom Tanzania Foundation ambapo tutatoa taarifa kuhusu huduma yetu ya m-mama inayowagusa kinamama kwa kuwapa usafiri pindi wanapopata dharura wakati wa kujifungua, pia tuna huduma ya E-Fahamu ambayo inatoa elimu kwa wanafunzi kwa njia ya kidijitali bila gharama yeyote.”

Aliendelea kusema, kampuni hiyo itatoa huduma ya M-Pesa inayowezesha kufanya huduma mbalimbali za fedha kidijitali kwa simu, VodaBima inayowezesha kupata huduma mbalimbali za bima ya magari na afya, pia wateja wetu watapata huduma ya Paisha App inayowezesha kupata mahitaji mbalimbali mtandaoni.

Pia Brigitta alisema, Vodacom imekuja na bahati nasibu ya Tusua mapene ambapo mteja anatakiwa kutuma neno V kwenda namba 15544 na anaweza kujishindia gari mpya aina ya Suzuki S Presso na pia kuna shindano la Tikisa litakalowezesha wateja wao kujishindia Smart Tv au shilingi milioni 1.

“Mwisho tunahuduma ya M-Kulima inayotoa taarifa mbalimbali za kilimo kidijitali kote nchini, hii itawezesha wakulima kujua pembejeo, bei za mazao, kulipa na kupokea pesa kwa M-Pesa”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...