Na.Khadija Seif, Michuzi

CHAMA cha Mashindano ya Magari (AAT) waendelea na Kampeni ya kuhakikisha wanafunzi Mashuleni wanapatiwa Elimu ya usalama barabarani pamoja na kuboresha Miundombinu ya alama za vivuko Ili kupunguza ajali kwa watoto.

Akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kuzindua rasmi Matembezi ya kilometa 30 kwa ajili ya kuhamasisha Elimu ya usalama barabarani Shule ya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam, Makamo wa Rais wa Kampuni ya Mbio za Magari (AAT) amesema wataendelea kutoa Elimu Kwa shule za Misingi na sekondari katika wilaya ya ilala na nyingine Ili kuhakikisha watoto wanafikia ndoto zao Kwa kuepuka ajali zisizo za lazima .

"Tutaendelea kushirikiana Kwa karibu na wadau mbalimbali wa usalama Barabarani kuhakikisha tunatoa elimu pamoja na vifaa vitakavyowezesha watoto mashuleni kuvuka barabara Kwa usalama zaidi."

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi na Afisa mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Meloe Buzema amesema endapo watumiaji wa barabara wataendesha kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa hususani katika maeneo masoko, Shule, Hospital na nyumba za ibada itasaidia kwa asilimia kubwa kupunguza ajali za barabarani.

Amesema kuwa, elimu iliyotolewa kwa wanafunzi hao itafika sehemu nyingi zaidi kwani watoto hao watakua mabalozi wazuri wa kutoa taarifa kwa jamii tofauti na kuzungumza kwenye vyombo vya habari kwani sio wote ambao wataweza kuona taarifa hiyo, hivyo kitendo kilichofanywa na Chama cha hicho ni mfano wa kuigwa na kwa wadau wengine.

"Jambo walilolipendekeza wenzentu hawa wa AAT ni zuri sana, kwani kuendesha kwa kasi ya 30 itapelekea barabara zetu kuwa salama zaidi kwani hata ikitokea kuna ajali imetokea haiwezi kuleta athari kubwa kutokana na mwendo uliotumika tofauti na mwendo kasi".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Chama Cha Mashindano ya magari (AAT) Najma Rashid amesema kuwa, wanategemea kuongeza uwelewa katika masuala ya usalama barabarani kupitia miradi yao na kufikia lengo la kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Aidha, amesema kuwa, wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo walimu wa shule za msingi na Sekondari, jeshi la Polisi pamoja na wanafunzi katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya barabara na kuepuka ajali zisizo za lazima lengo ikiwa ni kuhakikisha wanaweza kupunguza kasi ya uwendeshaji kutoka kilomita 50 kwa saa jadi kufikia kilomita 30.

Ameongeza kuwa, endapo kutakua na usimamizi mzuri wa kasi za uendeshaji kwa madereva barabarani itakua ni njia mbadala wa kuokoa maisha na majereha ya kudhoofisha kwani Uhusiano mkubwa kati ya mwendokasi na kifo hutumika na watumiaji wote wa barabarani.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Saady khimji ameikipongeza chama hicho kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali katika kuhakikisha wanatoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya usalama barabarani.

"Sisi kama Serikali, tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na chama cha Mashindano ya Magari (AAT) kwani wamekua wakitoa elimu ya usalama na kupelekea kupungua kwa ajali za barabarani tofauti na miaka ya nyuma, tunaomba na wadau wengine waweze kuiga mfano wao Ili tuhakikishe ajali za barabarani zinapungua".

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mnazi mmoja wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chama cha Magari (AAT) mara baada ya kuzindua rasmi Matembezi ya hisani ya kilometa 30 kwa lengo la kuhamasisha na kutoa Elimu ya usalama barabarani pamoja na kuboresha Miundombinu ya alama za vivuko kwa watoto Mashuleni katika jiji la Dar es salaam
Kamishna Msaidizi wa jeshi la polisi na Afisa mnadhimu wa kikosi cha usalama Barabarani ACP Meloe Buzema akizungumza na waandishi wahabari na kusisitiza kuwa chama cha AAT wanashirikiana Kwa karibu na jeshi la polisi kutoa Elimu ya usalama Barabarani kuhakikisha wanapunguza vifo vinavyosababishwa na ajali za Barabarani
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...