Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Maboresho ya Mazingira ya Biashara nchini, Dkt. John Jingu amesema Bajeti ya Serikali imefuta Tozo 232 ambazo zilikuwa changamoto kubwa kwa Wafanyabiashara kwenye Sekta mbalimbali nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika Kikao kazi cha Wadau wa Sekta Binafsi na Watendaji kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Pia Dkt. Jingu amesema Sheria na Kanuni mbalimbali zaidi ya 40 zimefanyiwa marekebisho ili kuhakikisha mazingira ya biashara nchini yanakuwa mazuri na bora.

“Bajeti imekuwa nyenzo muhimu kuboresha mazingira ya biashara nchini, kwa kiwango kikubwa Bajeti ya Serikali imeweza kushughulikia changamoto mbalimbali za biashara nchini”, amesema Dkt. Jingu.

Amesema mategemeo makubwa, Uchumi wa nchi utakuwa kwa kasi na Wafanyabiashara biashara hao kuchangamkia fursa ambazo zimetengenezwa na Serikali kupitia mifumo ya kikodi, Pia kuongezeka kwa Uwekezaji katika biashara mbalimbali kama biashara ya Mafuta.

Naye, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga amesema punguzo lolote la Kodi, limepunguza gharama za kufanya biashara na kuendelea kukuza uwekezaji nchini.

“Maboresho ambayo yamefanyika kupitia Bajeti ya Serikali ni kwamba Kodi, Tozo mbalimbali zimepungua na imesaidia sana kuuza Uwekezaji nchini na Biashara kwa ujumla, bei za bidhaa zinapungua na Walaji wataongezeka kwa sababu bei imepungua”, ameeleza Dkt. Wanga.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Paul Makanza amesema Wadau wa Sekta hiyo wanahakikisha wanaongeza kasi ya mazingira ya bidhaa nchini na kuchangia ukuaji wa Uchumi.

“Tumetoka kwenye athari za UVIKO-19, pia kuna Vita kati ya Urusi na Ukraine, sehemu mbalimbali duniani kumekuwa na athari za uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hauja mzuri hivyo kuongeza gharama. Hata hivyo Serikali kwenye Bajeti yake, ushuru na baadhi ya Malighafi zimepunguzwa”, amesema Makanza.


Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Maboresho ya Mazingira ya Biashara nchini, Dkt. John Jingu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maboresho ya Mazingira ya Biashara nchini na namna kukuza Uchumi wa nchi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga akizungumza kuhusiana na maboresho ambayo yamefanyika kupitia Bajeti ya Serikali ili kuweka mazingira wezeshi ya biashara nchini na kukuza Uchumi.

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Paul Makanza akizungumzia ushiriki wa Sekta hiyo katika kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Kikao kazi kilichoshirikisha Watendaji wa Sekta Binafsi na Taasisi mbalimbali za Serikali wakijadili namna kuweka mazingira bora ya biashara nchini na kukuza Uchumi wa nchi (Picha zote na Bakari Madjeshi)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...