Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, akitoa maelezo kwa Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo (kulia) alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Idara ya Majanga BoT, Bi. Dorosela Blasius na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay.
Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim
Msemo, akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la
Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, akifurahia jambo na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Joyce Shala na Afisa wa Benki Bi. Rukia Muhaji katika banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kibenki BoT, Bw. Augustino Hotay akifafanua jambo kwa
Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni,
walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.Mchambuzi
wa Masuala ya Kifedha BoT, Bi. Laila Kisombe akitoa elimu kuhusu
Uwekezaji katika Dhamana za Serikali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho
ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi kipya, Shilole akitazama picha za noti za Benki Kuu
ya Tanzania alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika
Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi. Beatrice
Ollotu.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma BoT, Bw. Lwaga Mwambande,
akielezea namna ya kutambua Alama za Usalama za noti zetu kwa wananchi
waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya
Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT, Bw. Elirehema Msemembo, akielezea sarafu za BoT kwa watoto waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...