Bibi yangu kipenzi Baraka bint Seif "Bi Kidude" nakuombea upumzike kwa amani, nimechelewa kuandika hii, lakini wakati wa Mungu ni wakati sahihi. Bibi umeitangaza Tanzania kimataifa, Nyenzo zako za kazi zikiwa muziki wa mwambao "Taarab" lugha yetu ya kiswahili na mavazi yako hasa magauni maarufu kama baibui, khanga ama yakushona ama zakujitanda.
Wageni nchi za nje waliijua zaidi Tanzania, lugha ya Tanzania na mavazi yetu asilia hasa Pwani kupitia wewe, hata uliporudi nyumbani, baadhi yao walikufuata kujifunza zaidi, BBC walirekodi habari zako na kuwahabarisha wengi huko duniani, bibi uliupiga mwingi. Huo ni upande wa matamasha ya nje, nchini taarab umeitambulisha, umeieneza na kuipa heshima, kazi gani ya serikali bila Bi Kidude, kumbi gani ya muziki bila Bi Kidude.
Bibi inawezekana huko ulipo ulikua unaumia kuona utamaduni wetu wenye yote hayo hauenziwi, usiumie tena, jibu limepatikana. Yupo waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Mohamed Mchengerwa, ametambulisha wiki ya utamaduni nchini Julai 1 mpaka 7. Rafiki yako Wane Star na wote wanaouenzi utamaduni wetu waziwazi watakuwakilisha, naskia kila kabila tutajua chakula chake cha asili, ngoma yake, mila na desturi zake.
Ukiacha wiki ya utamaduni, Mh Mohamed Mchengerwa na wizara yake wametambulisha wiki nzima yakiswahili, historia yakiswahili, ukuaji wake, mchango wake katika sekta tofauti nk. Pengine utajiuliza, utamaduni una wiki yake, Kiswahili kina wiki yake, Muziki wa mwambao viiipi..? Nao haujaachwa nyuma, una wiki yake, litafanyika tamasha kubwa katika fukwe za Coco beach DSM. Muziki wa mwambao unataka upepo, unataka nafasi, unataka mandhari ya pwani hasa bahari, vyoote vipo Coco beach hivyo.
\Bibi Insta wananizuia kuandika zaidi, lakini wajukuu zako ambao ni wanamuziki wameanza kupata mirabaha, upande wa soka nako mwache mwache, Serengeti girls na Tembo warriors wote wameenda kombe la dunia. Ningependa ujue mengi yanayoendelea bibi, lakini kwa kifupi ni hayo, pumzika kwa amani, wizara ya Utamaduni, sanaa na michezo inakuenzi huku.
Imeandikwa na James Tupatupa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...