Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa na uwekezaji mkubwa
uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan katika sekta ya elimu nchini.
Kauli hiyo imetolewa
leo Julai 21,2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM,
Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipotembelea Maonesho ya 17 ya
Vyuo Vikuu yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam.
Kabla
ya kutoa kauli hiyo Shaka alipata nafasi ya kutembelea mabanda
mbalimbali yaliyokuwepo kwenye Maonesho hayo na kisha akatoa maelezo
kuhusu na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya
elimu nchini ukiwemo Wizara ya elimu na Taasisi zake.
"Katika
elimu kuna uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ambao
unaendelea kutoa matunda mazuri katika sekta hii na Chama chetu
kinaridhishwa sana,"amesema Shaka na kuelezea hatua kwa hatua
yanayoendelea kufanywa na Serikali ili kuendelea kuiboresha zaidi ya
sekta ya elimu.
“Nimetembelea mabanda ya taasisi mbalimbali za
elimu zinazoshiriki maonyesho haya, nimejionea na kusikia mambo makubwa
ya maendeleo,” ameeema na kuongeza katika bajeti ya mwaka huu ongezeko
la fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na
wizara nzima ya elimu, ni hatua muhimu iliyotengeneza mazingira rafiki
kwa sekta ya elimu,"amesema Shaka.
Akielezea zaidi Shaka amesema
huko nyuma kulikuwa na malalamiko mengi aliyokuwa akiyapokea ofisini
kwake kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, yaliyomlazimu
kutembelea Bodi ya Mokopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na sasa
hali imeimarika.
Amefafanua kwamba Rais Samia amefanya kazi kubwa
katika sekta ya elimu katika kipindi cha mwaka mmoja na moja ya mambo
ambayo hayazungumzwi sana ni namna alivyosamehe deni la karibia Sh.
trilioni 1.1 ambalo lilikuwa halilipiki kwa bodi hii ya mikopo.
Aidha
Shaka amesema Sh.bilioni 985 ambazo zimetengwa katika bajeti ya
2022/2023 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vikuu, kuwapatia mafunzo
ya taaluma wahadhiri na kununua vitendea kazi itazidi kutengeneza
mazingira mazuri kufundisha na kujifunzia.
“Azma na utayari wa
Rais Samia kuibeba sekta hii ya elimu sote tumekuwa mashuhuda, name
nataka niwaambie kuwa ameanza vizuri, tunaamini uboreshaji huu
utaendelea."
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo
Vikuu (TCU), Profesa Charles Kihampa amesema wanaishukuru Serikali ya
CCM kwa kuendelea kuitazama kwa karibu sekta ya elimu nchini na kwamba
katika kipindi cha mwaka mmoja madarakani, uwekezaji mkubwa umefanywa a
na Rais Samia katika elimu.
Amesema uwekezaji huo umechochea
ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa kwa ajili ya elimu ya juu kutoka
wanafunzi 8,7934 hadi 100,620.Aidha Profesa Kihampa amemueleza Shaka
kuhusu juhudi zinazoendelea katika kuboresha elimu na taaluma
inayotolewa na Vyuo Vikuu nchini.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipokewa na Viongozi waandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof Charles Kihampa pamoja na Mkurugenzi Udahili na Menejimenti ya Data Dkt.Kokuberwa Mollel wakati akiwasili leo Julai 21,2022 katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza mbele ya waandishi wa vyombo vya habari mara baada ya kutembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Julai 21,2022 mkoani Dar es Salaam.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof Charles Kihampa alipotembelea kwenye moja ya banda la Wakala wa Masuala ya elimu kutoka nchini India,wakati akitembelea Maonesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Julai 21,2022 mkoani Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...