Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi wakati wa mkutano mkuu wa umoja huo ulifanyika mkoani Iringa




Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
cha walimu Tanzania (CWT) imeitaka serikali kukirudisha kikokotoo
kilichopendekezwa kwa wadau ili kijadiliwe kwa kuwa sasa kinawaumiza
wafanyakazi pale wanapoenda kustaafu.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa umoja wa viongozi wa chama
cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na
Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi,Katibu wa
chama cha walimu mkoa wa Iringa (CWT),Hamisi Chinahova alisema kuwa walimu
wamekuwa wakifanya kazi kwa kujitolea muda wote kwa kulijenga taifa hili.
Chinahova alisema kuwa walimu wamekuwa wanafanya kazi kwa weledi
mkubwa kuhakikisha wanawafundisha Wanafunzi kwa juhudi kubwa hivyo serikali
inatakiwa kukiangalia upya kikokotoo hicho.
Alisema kuwa walimu wanakumbana na mazingira duni ya kufanyia
kazi ikiwapo pamoja upungufu wa vifaa vya kufundishia
Chinahova alisema kuwa walimu wamekuwa wanadai madeni mbalimbali
na ya muda mrefu hivyo wanaiomba serikali kuhakikisha wanatatua changamoto ya
madai ya walimu ili waendelee kufanya kazi wito kama awali.
Alisema kuwa watumishi walimu wasipangiwe bank ya kutumia
kupitisha mishahara yao kwa kuwa hiyo ni haki ya msingi na serikali inapaswa
kuridhia swala hilo.
Chinahova alimazia kwa kusema kuwa serikali inatakiwa kuendelea
kuajiri walimu wengi sambamba na ujenzi wa madarasa ili kuwapunguzia changamoto
walimu wakiwa kazini.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo,mkuu wa wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa chama cha walimu Tanzania kinafanya
kazi kubwa ya kuishauri serikali juu ya upatikanaji wa ajira za walimu ili
kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu.
Moyo alisema kuwa walimu wamekuwa chachu ya mabadiliko ya muundo
wa serikali juu ya watumishi ili kuhakikisha watumishi wanapata haki zao za
msingi.
Alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa italifanyia kazi haraka
swala la kuwarudisha wastaafu mapema makwao mara baada ya kustaafu kwa kuwa
wamelitumikia taifa hili kwa miaka yao yote ya utumishi ambapo wamechangia kwa
kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania.
Moyo alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto ya
miundombinu ya shule na vifaa vya kufundishia na kujifunzia kadri fedha
inavyopatikana.
Alimazia kwa kusema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
imeanza kufanya maboresho kwenye sekta ya elimu na kuonyesha nia yake ya
kuendelea kuboresha sekta hiyo.
Nao baadhi ya wenyeviti wa CWT nyanda za juu kusini walisema
kuwa kufanya kazi kwa ushirikiano ndio jambo ambalo litasaidia taasisi hiyo
kukua kila wakati.
Walisema kuwa mshikamano kazini ndio kitu bora kwa wafanyakazi
walimu kuendelea kutunza nidhamu kazi kwa kuwalea watoto katika maadili
yanayotakiwa.
Walisema kuwa walimu ndio wamekuwa chanzo cha maendeleo ya
nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kuwa viongozi bora kwenye sekta
mbalimbali.
Waliongeza kwa kusema kuwa walimu ni wito jambo ambalo limekuwa
kukisaidia kuzalisha wasomi wengi wenye tija ya kimaendeleo.
Walisema kuwa walimu wanapaswakutimiza wajibu wao kama
inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria zote za kazi na nini katiba ya nchi
inavyosema.
Lakini pia mkuu wa wilaya ya Momba Faki Lulandala aliwataka
viongozi wa CWT kutetea maslai ya wafanyakazi walimu ili kuendeleza umoja na
maslai ya walimu.
Lulandala alisema chama cha walimu ndio chama kikubwa kuliko
vyama vyote vya wafanyakazi Africa kutokana na umoja na mshikamano uliopo licha
ya mara kadhaa kukumbana na changamoto mbalimbali.
Alisema kuwa utulivu na mshikamano uliopo hapa nchini unatokana
uongozi wa CWT kuwa umoja na utulivu uliopo hivyo viongozi wanapaswa kuendelea
kudumisha utamadumi uliopo toka zamani.
.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...