Na mwandish wetu


Dar es Salaam. Kampuni ya kuunganisha magari nchini, GFA leo imeunganisha gari la 600 ikiwa ni miaka miwili tangu ianze shughuli hiyo Septemba mwaka 2020.

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 15 ya kampuni hiyo, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji, amesema kiwanda hicho kimeifaya Tanzania kutimiza moja ya itifaki za kuwa katika eneo huru la biashara Afrika.

"Tulikuwa wapokeaji lakini hatukuwa na kiwanda cha kuunganisha magari, GF Truck imetufanya tuwe na cha kusema tunapoingia katika vikao vya kiitifaki vya eneo huru la biashara la Afrika," amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GF Trucks, Imran Karmari alisema kampuni hiyo ilianza kuunganisha gari la Kwanza Septemba 2020 na hadi sasa imeshaunganisha magari 600.

"Mara ya kulikuwa na mashaka kwamba Watanzania tutaweza na bidhaa zitakuwa na ubora, lakini hadi hatua hii tumeweza," amesema.
Kampuni  ya GF Trucks & Equipment’s Ltd ilianza mwaka 2007 ikiwa na wafanyakazi wanne na haikuwa na ofisi.
Alisema kwa sasa asilimia 80 ya malighafi za kuunganisha magari wanaagiza kutoka China huku asilimia 20 pekee ndiyo zinazotoka ndani.

"Bado Tanzania hakuna Viwanda vya malighafi ya kuunganisha magari ndiyo maana tunaagiza, lakini mipango yetu ya baadaye ni sisi wenyewe kuanzisha kiwanda," alisema.

Hata hivyo, alisema jumla ya watu 300 wameajiriwa moja kwa moja katika kampuni hiyo yenye makao makuu yake Kibaha mkoani Pwani.

Tunajivunia kuwa  Kampuni ya kwanza nchini kuwa na kiwanda cha kunganisha magari na  wakati tunaanza hatukutegemea kama tutafika siku kama leo kutikiza idadi ya magari 600.
Pia lengo la kampuni ni kuweza kuunganisha magari ya aina zoote ingawa kwa sasa tunaunganisha Truck pekee na tunashukuru FAW  na HONG YANG kwa kutuamini na kuweza kunganisha magari katika kiwanda chetu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...