KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Eliamani Sedoyeka Leo Julai 04, 2022 ametembela banda la TAWA lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Kibiashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la TAWA Prof. Sedoyeka alipata  maelezo mahsusi kuhusu Hifadhi za Magofu ya kale  kunduchi ambayo yako chini ya Usimamizi wa TAWA kutoka Kwa Mhifadhi Mwandamizi Jasmin Mushi

Pia alitumia fursa hiyo kutembelea bustani ya Wanyamapori hai na kujionea Wanyamapori mbalimbali waliopo katika bustani hiyo ikiwa ni pamoja na kupata maelezo kutoka Kwa maofisa wa TAWA kuhusu tabia za Wanyamapori hao.

Prof. Sedoyeka ametumia fursa ya ujio wake kwenye maonesho hayo  kuhamasisha wananchi kuendelea kutembelea banda la Wizara ya Maliasili  na Utalii  kujionea shughuli  mbalimbali zinazofanywa na wizara na taasisi zake pamoja na wadau mbalimbali katika masuala ya  uhifadhi wa Maliasili, Malikale  na Uendelezaji Utalii.

"Watu wote watakaofika katika banda letu la maliasili hapa sabasaba watapata huduma za  chakula kutoka chuo cha Taifa cha Utalii lakini kikubwa watapata kuona wanyamapori mbalimbali wakiwemo chui, fisi, mamba na aina mbalimbali za wanyamapori wanaotambaa kama kobe na nyoka wakubwa"




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...