MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa jumla ya mashahidi 54 wanatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya mbili kati ya tatu za uhujumu uchumi zinazomkabili Mkurugenzi wa zamani wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (Udart) Robert Kisena na wenzake.
Pia vielelezo 153 ambavyo vitajumlisha mambo mbalimbali ikiwemo mikataba mbalimbali hati za makubaliano, hati za kuamuru utoaji wa vielelezo, taarifa za ukaguzi wa hesabu nyaraka za benki na hati za udhamini navyo vitatolewa wakati wa ushaidi katika kesi hizo mbili.
Kesi hizo mbili namba 20 na 21 za mwaka 2022 dhidi ya Kisena na wenzake zilifunguliwa mahakama ya Kisutu katika hatua ya uchunguzi na leo Julai 28,2022 washtakiwa wamesomewa maelezo ya mashahidi.
Hatua hiyo imekuja imekuja baada ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo kukamilika na upande wa mashtaka leo Julai 27, 2022 kuwasilisha mahakamani maelezo ya mashahidi na vielelezo vitakavyotumika wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo Mahakama Kuu kitengo cha mafisadi.
Imeelezwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Ladislaus Komanya kuwa katika kesi namba 20 ya mwaka 2022 iliyokuwa inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo, upande wa mashtaka unatarajia kuwaita mashahidii 24 na kuwasilisha vielelezo 58.
Vielelezo hivyo ni nyaraka mbalimbali zikiwemo taarifa za benki (bank statements) mikataba waliyoingia washtakiwa na kambuni mbalimbali, maelezo ya maandishi ya mashahidi na ya washtakiwa, na hati za ukamatwaji wa washtakiwa na za upekuzi.
Katika kesi hiyo Kisena (47) ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Simon Group Ltd anashtakiwa pamoja na Charles Newe ( 48) mkurugenzi wa Udart, mfanyabiashara John Samangu ( 66) na mtunza fedha wa Udart, Tumaini Kulwa( 44).
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 15, ambayo ni kuongoza genge la uhalifu na kughushi, kuwasilisha nyaraka za uwongo, utakatishaji fedha haramu na kuisababishia Udart hasara ya Sh750 milioni, wakidaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, Mei 25 na Julai 10, 2016.
Pia katika kesi namba 21 ya mwaka 2022 iliyokuwa inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Godfrey Isaya, upande wa mashtaka unatarajia kuwaita mashajidi 30 na kuwasilisha vielelezo vya nyaraka mbalimbali 95.
Katika kesi hiyo mbali na Kisena, Newe, Samangu na Kulwa, mshtakiwa mwingine ni mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Africa (maarufu kama Maxmalipo, Juma Furaji (48).
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 22, yaani kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uwongo, utakatishaji fedha haramu na kuisababishia Udart hasara ya Sh4, 505,125, 000 (zaidi ya Sh4.5 bilioni).
Hatua hiyo ya leo imehitimisha jukumu la mahakama hiyo na kufunga majaladq ya kesi hizo huku ikiamuru kesi zihamishiwe Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambayo ndio ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi za aina hiyo.
Hakimu Isaya amewaeleza watuhumiwa kuwa wataendelea kuwa mahabausu mpaka pale shauri hilo litakapoitishwa kwenye Mahakama Kuu divisheni ya Rushwa na Makosa ya Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...